Meneja
wa bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga akizungumza na waandishi
wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Simu janja aina ya
Samsung Note 20 na Samsung Note 20 Ultra.Kushoto kwake ni Mkaazi Samsung
electronics Tanzania. Suleiman Mohamed Hafla ya uzinduzi imefanyika leo
katika makao makuu ya Tigo Jijini Dar Es Salaam.
Meneja
Mkaazi Samsung electronics Tanzania Suleiman Mohamed akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Simu
janja aina ya Samsung Note 20 na Samsung Note 20 Ultra.Kulia kwake ni
Meneja wa bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga Meneja
wa bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga akieleza sifa za Simu
janja aina ya Samsung Note 20 na Samsung Note 20 Ultra mara wakati wa
uzinduzi wa simu hizo mapema leo jijini Dar es salaam.Anayeshuhudia
pembeni ni Meneja Mkaazi Samsung electronics Tanzania Suleiman Mohamed .
====== ======== ==========
Wateja watakaonunua simu hiyo watajipatia Gb78 za intaneti kwa mwaka mzima
Kampuni
inayoongza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo kwa kushirikiana na
Samsung Electronics wamezindua Simu janja aina ya Samsung Note 20 na
Samsung Note 20 Ultra.
Ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati wa
Tigo wa kuongea matumizi ya mtandao wa 4G na kuchangia ukuaji wa
teknolojia ya kidigitali nchini.
Meneja wa bidhaa za intaneti wa
Tigo, Mkumbo Myonga akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo alisema
“Ni jambo la kubwa sana kwetu kuchaguliwa na Samsung kuwa wa kwanza
kuzihifadhi na kuuza simu za Samsung Note 20 na Samsung Note 20 ultra
kwenye soko la Tanzania.Hii inaonesha imani yao kwetu juu ya chaneli
kubwa za usambazaji tulizonazo na pia kupitia timu yetu ya huduma kwa
wateja inayotoa huduma zenye ubora wa hali ya juu,”alisema Myonga.
“Lengo
letu ni kuchochea mageuzi ya kidigitali katika maisha ya watu hapa
nchini na ndio maana tumeungana na Samsung ili kuongeza idadi ya umiliki
wa simu janja pamoja na matumizi ya data ili kuhakikisha watu wengi
zaidi wanaifikiwa na teknolojia hii,” alisema Muyonga.
Muyonga
aliongeza “Tunalenga kuongeza ueneaji wa simu janja nchini huku
tukihakikisha wateja wetu wanafurahia huduma za kidigitali kupitia
mtandao mkubwa wa 4G hapa nchini.Na ndio maana tunatoa 78 Gb za intaneti
kwa mwaka mzima kwa wateja wote watakaonununa Samsung Note 20 na
Samsung Note 20 Ultra,” alisema .
Akizungumza wakati wa uzindizu
huo, Meneja Mkaazi wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohamed alisema Samsung
imezindua simu ya Samsung Note 20 na Samsung Note 20 ultra toleo jipya
ulimwenguni ambayo itabadilisha namna ambavyo watu wanavyoishi na
kuufurahia ulimwengu.
“Tukiwa tunaingia kwenye muongo mwingine,
kuna mabadiliko makubwa kwenye sekta ya mawasiliano na namna watu
wanavyo ujua na kuufurahia ulimwengu.Samsung inahakikisha inatoa
teknolojia na vifaa vya kisasa zaidi ili kuendana na mabadiliko hayo.Kwa
kutumia camera yenye mfumo wa AI unaweza kupata kila tukio na kuungana
na uwapendao bila mipaka,” alisema Mohamed.
Simu ya Samsung Note 20 itauzwa kwa Sh2,480,000, na Samsung Note 20 Ultra kwa sh 3,185,000.
|
No comments :
Post a Comment