Mkuu
wa Wilaya ya Karatu Abbas Kayanda (kulia) akimkabidhi Mwalimu mstaafu
Mzee Pilonga Vicent juzi million 21 na laki moja ,Fedha zilizookolewa
na Takukuru Wilaya ya Karatu Mara baada ya mstaafu huyo kuporwa na
kampuni ya Robby credit Company limited inayomilikiwa na Emmanuel
Bonifasi tangu February Mwaka 2019 wengine katika Picha Ni maafisa wa
Takukuru.(Picha na Woinde Shizza, KARATU).
Na Woinde Shizza ,Michuzi TV Arusha
TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Karatu imeokoa
kiasi cha shilingi million 21 na laki moja za Mwalimu Mstaafu, Fedha
hizo zilikuwa zimeporwa na kampuni ya Robby credit Company limited
inayomilikiwa na Emmanuel Bonifasi tangu February Mwaka 2019.
Mkuu
wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda alisema Mzee Pilonga Vicent alienda
kukopa fedha kwenye taasisi ya kifedha ya Robby credit kiasi cha million
3 kwa makubaliano ya kurudisha kiasi cha fedha hizo na riba ya 30%
ambapo baada ya kuingia kwa fedha yake ya kustaafu million 25 fedha zote
zilichukuliwa na taasisi ya Robby credit.
Kayanda
alisema vyombo vya habari vimemsaidia kujenga elimu ya uelewa Mzee
Pilonga juu ya namna taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa inaweza
kumsahidia ,hata ikafanya aweze kwenda kutoa taarifa Takukuru
Aidha
alisema Takukuru walichunguza kwa undani jambo la Mzee Pilonga na
kugundua kwamba taasisi ya Robby credit ilichukua kadi ya bank na pamoja
na numba yake ya siri , hiyo ilichangia fedha za Mzee Pilonga
kuchukuliwa na taasisi ya Robby credit.
Kayanda
alibainisha watendaji wa Takukuru walilisimamia jambo hilo na viongozi
wa Robby credit walikiri makosa waliyoyafanya na kurudisha fedha hizo
Alitoa
wito kwa wananchi ambao wamedhulumiwa katika taasisi za kifedha na
wanaushahidi wawasilishe malalamiko katika taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa ,hata wananchi wanaoenda katika taasisi za umma
kupata huduma, kama kuna vitendo vyovyote vinavyoashiria rushwa wasisite
kutoa taarifa Takukuru ili kudhibiti vitendo vinavyoharibu taswira ya
utendaji kazi.
Awali
katika taarifa yake Naibu wa takukuru mkoa wa Arusha Sabasi Salehe
alisema matatizo hayo yamezidi kuongezeka mkoani Arusha na wameanza
kurejesha fedha nyingi, aliongeza hushughulikia watuhumiwa kwa njia
mbili kwanza kwa kuchunguza kwa kina na kujiridhisha kama Mtuhumiwa
aliyefanya alifanya pasipokujua, kama ni kweli akirejesha fedha
alizochukua anasamehewa na kuonywa.
Alisema kuna watuhumiwa ambao wanavunja sheria ya Takukuru No1 ya mwaka 2017 hivyo sheria inachukuliwa dhidi yao
Kamanda
wa Takukuru wilaya ya Karatu Atuganile Stephen alisema wananchi wenye
mikopo umiza watoe taarifa ofisini ikiwa ni pamoja na watu wenye taarifa
za vitendo vya rushwa kwani jukumu la kupambana na rushwa ni letu sote
.
Naye
mtaafu aliyerejeshewa fedha zake Mzee Pilonga alisema anajisikia amani
yake imerejea kwa sababu alikuwa anawaza analeaje familia kutokana na
unyang’anyi haliofanyiwa, lakini kutokana na juhudi za serikali kupitia
Takukuru fedha zake zimepatikana, Mzee Pilonga ameishukuru sana
serikali kwa msaada aliopata.
No comments :
Post a Comment