
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango Dotto James,akizungumza kwenye Mkutano wa kupokea Ripoti ya
Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali
(GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.


Sehemu ya Wadau wakifatilia hotuba
ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James,(hayupo pichani)
wakati akizungumza kwenye Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo
wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG)
iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii Bw.William Erio,akitoa taarifa ya mrejesho kutoka
taasisi zinazotumia Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya
Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Mhandisi Mwandamizi Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam akitoa wasilisho la Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa
Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika
leo jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu,Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw.Alexander Sanga,akielezea mrejesho
kutoka taasisi zinazotumia Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa
Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Mhasibu Mkuu kutoka Taasisi ya
Wakala wa Huduma ya Hifadhi za Msitu Tanzania,Peter Mwakosya,akizungumza
kwenye Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki
wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini
Dodoma.

Mchambuzi wa Sera kutoka TARURA
Dk.Noel Komba,akizungumza kwenye Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini
ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG)
iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Mhasibu Mwandamizi ,Edward Michael
kwa niamba ya Mkurugenzi Mtendaji Benjamini Mkapa Hospital ,akizungumza
kwenye Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki
wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini
Dodoma.

KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango Dotto James,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea
Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya
Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali kupitia Wizara
ya Fedha na Mipango inatarajia kuanza kutoa elimu ya matumizi ya malipo
ya Serikali kwa njia ya Mtandao GePG kwa wananchi ili kuongeza uelewa
kwa jamii juu ya matumizi ya mfumo huo mpya ambao umeleta mafanikio
katika kukusanya mapato ya
Serikali.
July 2017 Serikali
ilizindua rasmi mfumo wa malipo ya makusanyo ya serikali kwa njia ya
mtandao Government Electronic Payment Gateway GePG ambapo makusanyo yote
ya Halmashauri na Taasisi za kiserikali hutumia kukusanya mapato yake.
Kauli hiyo imetolewa leo
jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James
wakati wa Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa
Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) amesema kuwa
mfumo huo umekuwa na mafanikio katika kukusanya mapato.
Bw.Jamese amesema kuwa
mfumo huo bado umekuwa changamoto kwa wananchi hasa uelewa Kati ya GePG
na Control number wengi wamekuwa wanashindwa kutofautisha.
” Wananchi wengi
wanatumia mfumo huu na unawasaidia lakini wengi hawaelewi maana ya GePG
na Control number wengi wanasema nimetuma kwa kutumia Control number
tutapita maeneo mbalimbali kutoa elimu hiyo wajue” amesema Dotto James.
Hata hivyo amesema kuwa
mfumo huo umerahisisha kazi katika maeneo mbali mbali ambapo umesaidia
kuondoa changamoto nyingi na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali
na mfumo huo Sasa unatumiwa na taasisi zaidi ya mia sita (600).
Amebainisha kuwa tangu
kuanza kwa mfumo huo ukusanyaji wa mapato ya Serikali umeimarika Sana
hadi kufikia asilimia 250 na kuondoa mianya ya upotevu wa mapato ya
Serikali.
” Kabla ya mfumo huo
tulikuwa tunakusanya bilioni 688 lakini kwa Sasa baada ya kuanza kwa
mfumo huu tumefikia tilioni 2.6″ amesema.
Aidha ameonya kwa
taasisi na halmashauri zote hapa nchini kutoanzisha mfumo wowote bila
idhini ya Waziri wa Fedha na Mipango ili kudhibiti uanzishwaji wa mifumo
kiholela.
Amesema Wizara imeweza
kutengeneza mifumo minne katika Kudhibiti mapato ya Serikali na
imeanzisha GePG, mfumo wa usimamizi wa matumizi ya Serikali MUSE, Mfumo
wa usimamizi wa miradi ya maendeleo (kanzi data ya miradi ya maendeleo)
na mfumo wa usimamizi wa misamaha ya kodi ya miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na Serikali.
Awali Mhadhiri
mwandamizi Chuo Kikuu Cha Dar es saalam (UDSM),Prof.Dkt Joel Mtebe,
amesema kuwa wamefanya utafiti kuhusu mfumo huo na kubainisha kuwa
umekuwa msaada na kuwezesha ukusanyaji mzuri wa mapato ya Serikali.
“Tumepita maeneo mengi
tumeona imekuwa msaada mkubwa na umedhibiti upotevu wa mapato ya
Serikali na kuwawezesha watumishi katika maeneo yao kufanya kazi kwa
wakati” amesema Dkt Mtebe.
No comments :
Post a Comment