Leo Septemba 29, 2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli amemteua, Dkt. Eblate Ernest Mjingo kuwa Mkurugenzi Mkuu
wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI).
Kabla ya uteuzi
huo, Dkt. Mjingo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Tiba ya Wanyamapori na
Huduma za Maabara wa TAWIRI, na anachukua nafasi iliyoachwa na Dkt.
Simon Mduma ambaye amestaafu.Uteuzi wa Dkt. Mjingo unaanza leo tarehe 29 Septemba, 2020.
No comments :
Post a Comment