Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imekutana na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni ‘Online Content Service
Providers’ nchini Tanzania kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya
mchakato wa uchaguzi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 28,2020.
Mkutano huo umefanyika leo Jumanne
Septemba 15,2020 katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius
Nyerere, jijini Dar es salaam .
Akifungua Mkutano huo, Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles amesema
Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni ni wadau muhimu katika mchakato wa
uchaguzi ndiyo maana wameamua kukutana nao ili kuwajengea uwezo kuhusu
masuala ya uchaguzi ili waweze kuandika habari kwa usahihi na kulinda
amani ya nchi.
“Tume ya Taifa ya Uchaguzi
tunavipongeza vyombo vya habari mtandaoni kwa ushirikiano ambao mmekuwa
mkitupatia.Tunathamini mchango wenu na tutaendelea kushirikiana nanyi
ili kujenga nchi yetu. Tumewaita ili kuwajengea uelewa kuhusu mkachato
wa uchaguzi,tunaamini kuwa mna nafasi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusu
taratibu mbalimbali za uchaguzi”,amesema Dkt. Charles.
Aidha amewataka waandishi wa habari
kuvipa nafasi sawa vyama vyote vya siasa na kuepuka kuandika habari
zenye kuhamasisha vurugu na kusababisha uvunjivu wa amani.
“Kipindi cha Kampeni za uchaguzi huwa
kuna joto la uchaguzi ambapo joto la kuvunja amani nalo huongezeka.
Naomba tulinde amani ya nchi yetu kwa kuepuka kuandika habari zenye
kuleta chuki”,amesema.
Katika hatua nyingine alivitaka vyama
vya siasa kufuata maadili ya uchaguzi na sheria za nchi na kuhakikisha
wanafanya kampeni za kistaarabu huku akivikumbusha vyombo vya habari
kuepuka kuandika kauli na matamshi ya kuvunja amani.
“Kuanzia sasa tutachukua hatua kali
kwa viongozi wanaotoa matamshi ya kuvunja amani. Hata wewe mwandishi wa
habari ukiandika habari zenye kuunga mkono matamshi hayo nawe utakuwa
unavunja amani”,ameongeza Dkt. Charles.
Dkt. Charles ametumia fursa hiyo
kuviomba vyombo vya habari kuelimisha jamii kushiriki katika mchakato wa
uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye
mikutano ya kampeni kusikiliza sera za wagombea na kupiga kura Oktoba
28,2020 ili kupata viongozi wanaowataka watakaowaletea maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma, ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Asina Omari, amesema.
"Vyombo vya Habari mitandaoni vina nguvu kubwa katika masuala ya siasa hivyo ni muhimu watoa huduma ya habari mtandaoni kuhakikisha mnatumia vyanzo sahihi vya habari ili habari Mnazoziandika ziwe sahihi,Habari zitoke kwenye vyanzo sahihi ili habari ziwe sahihi”.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma, ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Asina Omari, amesema.
"Vyombo vya Habari mitandaoni vina nguvu kubwa katika masuala ya siasa hivyo ni muhimu watoa huduma ya habari mtandaoni kuhakikisha mnatumia vyanzo sahihi vya habari ili habari Mnazoziandika ziwe sahihi,Habari zitoke kwenye vyanzo sahihi ili habari ziwe sahihi”.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa
Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya
Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati akifungua Mkutano kati ya
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari
Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera
Charles akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo
pichani),wakati akifungua Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma,
ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Asina Omari
akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo
pichani),wakati wa Mkutano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC),uliofanyika leo katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius
Nyerere, jijini Dar es salaam .
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu kwa Mpigakura, Giveness Aswile
akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo
pichani),wakati wa Mkutano huo kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
"Vyombo vya Habari mitandaoni vina nguvu kubwa katika masuala ya siasa
hivyo ni muhimu watoa huduma ya habari mtandaoni kuhakikisha mnatumia
vyanzo sahihi vya habari ili habari Mnazoziandika ziwe sahihi,Habari
zitoke kwenye vyanzo sahihi ili habari ziwe sahihi”, alisema Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma, ambaye pia ni
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Asina Omari.
Baaadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kahama Tv Online, Shija Felician na Mkurugenzi wa Malunde Media, Kadama Malunde wakiwa kwenye Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni
Sehemu ye Meza kuu
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.
No comments :
Post a Comment