Wednesday, September 30, 2020

MWANAMKE WA KITANZANIA AISHIE MAREKANI AANDAA KONGAMANO LA KUWAFUNZA WAFANYABIASHARA WANAWAKE WA KITANZANIA


Mwanamke Mtanzania mfanyabiashara aishiye Marekani(UK) ,Gladness Katega akiongea na waandishi wa habari juu ya kongamano la wanawake wafanyabiashara aliloliandaa.

………………………………………………………..

Na Woinde Shizza,Arusha
Mwanamke Mtanzania mfanyabiashara aishiye Marekani(UK) ,Gladness Katega Amewataka wanawake  kujitokeza katika kongamano la wajasiliamali linalotarajiwa kufanyika mnamo Oktoba 2 na 3 ili kujifunza na kujadili changamoto za kibiashara ili kuweza kupanua biashara zao na kumuinua mwanamke kiuchumi.
Aidha pia Alisema kuwa mbali na wanawake pia litakuwa na kongamano lingine ambalo litafanyika October 5 na 6 ambalo litawakutanisha wanaume na kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Katega alisema kongamano hilo litawasaidia  wanawake wa Tanzania katika kuinuka kiuchumi na kuweza kutanua biashara zao
Alibainisha kuwa   lengo  lao kubwa la kufanya kongamano hili ni  kuwaweka wanawake pamoja na kuona wanafanya biashara kwa pamoja na kuinuka
Alisema kuwa kongamano hilo litashirikisha wanawake hapa nchini pamoja na nchi mbalimbali ikiwemo Marekani ,Uingereza,Ghana ,Zimbabwe , Southafrika pamoja na Kenya na hasi Sasa zaidi ya wanawake 100 wameshathibitisha kishiriki
Alisema kuwa wanataka kuona mwanamke anainuka   kiuchumi anatoka hatua moja anaenda hatua nyingine  na anafanikiwa na pia napenda kuona wanawake wakibebana wakisaidiana ili waweze kufika mbali na kongamano hili litawasaidia kupata elimu watapata  mafunzo watajadiliana namna ya kukuza biashara nakufikia Mataifa mengine
Alisema  mgeni rasmi wa kongamano hili  anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira huku akitaja wathamini wa kongamano hili kuwa ni  Burka Coffee Logle ,Duluti garden,Mrembo safari,TTB,sunbright hotel,partner Africa Investment,na Kipina beauty saloon .
Alitoa wito kwa Kila mwanamke na mwanaume kuhuthuria ili  kuweza kupata  mitandao ya kibiashara nakujua namna ya upatikanaji wa masoko pamoja na kutatua changamoto ya namna ya kukuza biashara zao ,pamoja nanamna ya kufanya biashara kimataifa ukizingatia katika kipindi hichi ambacho baadhi ya nchi bado zinakabiliwa na janga la ugonjwa wa covid 19
Naye  mwezeshaji wa mfunzo ya wanaume ya Kings master class kutoka nchini Kenya ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya RB, Dk.Robert Burale alisema wanaume wengi wanatunza  maumivu moyoni na kushindwa kuyasemea kwa watu kuhusu hali ya maisha pamoja na changamoto ambazo wanakutana nazo Ndani ya familia  kitu ambacho hufanya baadhi ya wanaume kupoteza maisha na wengine kufanya maamuzi ambayo Sio mazuri

“mwanamke anaweza akapata kitu akachukuwa sumu akanywa ,au hata akajinyonga  lakini kwa mwanamme anaweza akaumizwa na kitu badala ya kufikiria kijinyonga yeye akachukuwa uamuzi wa moja kwa moja hivyo nitawaeleza namna ya kukabiliana na changamoto hiyo “alibainisha

Aliwataka wanaume kujitokeza kwa wingi katika kongamano hili ,huku aliwasisitiza wanawake kuwashauri wanaume wao kwenda katika kongamano ,kwani iwapo watajitokeza hawata jutia .

 

No comments :

Post a Comment