Baadhi
ya akinamama wakifuatilia mafunzo juu ya namna bora ya kunyonyesha
sambamba na suala zima la malezi ya mtoto, mafunzo hayo yaliyofanyika
mjini Musoma jana ambayo yakiitwa Mother Meet Up event huku yakiandaliwa
na Shirika la FHI360 chini ya ufadhili wa Shirika la misaada la
Marekani la USAID.
Baadhi
ya akinamama wakifuatilia mafunzo juu ya namna bora ya kunyonyesha
sambamba na suala zima la malezi ya mtoto, mafunzo hayo yaliyofanyika
mjini Musoma jana ambayo yakiitwa Mother Meet Up event huku yakiandaliwa
na Shirika la FHI360 chini ya ufadhili wa Shirika la misaada la
Marekani la USAID.
Mratibu
wa Huduma za mama na mtoto Manispaa ya Musoma, Deborah Mkama
akimuelekeza mama jinsi ya kumnyonyesha mtoto wakati wa mafunzo ya namna
ya unyonyeshaji ya Mother Meet Up Event yaliyoandaliwa na Shirika la
FHI360 chini ya ufadhili wa Shirika la misaada la Marekani la USAID
mjini Musoma jana.
Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na Rorya mkoani Mara zanufaika na
mradi wa USAID Tulonge Afya unaolenga kutoa elimu katika jamii ili kubadili tabia hasi ili kuweza kuisaidia jamiii kuwa na Afya njema..Akizungumza
mjini hapa jana kwenye shughuli ya wakina mama wenye watoto chini ya
miezi sita ijulikanayo kama “Mother Meetup” iliyoandaliwa na na mradi wa
USAID TULONGE AFYA kupitia jukwaa la NAWEZA kwa lengo la kuwakumbusha
wakinamama hao juu ya malezi bora ya watoto .
Mratibu
wa asasi ya OWSL, Dk. Theophil Kayombo dhumuni la kuwakutanisha kina
mama hao ni kuwapa nafasi ya kuweza kupeana uzoefu na kujadiliana mambo
mbalimbali yahusuyo malezi ya watoto kuanzia wanapozaliwa mpaka kufikia
umri wa miaka mitano.
Aidha
Dkt, Kayombo aliainisha mambo hayo kuwa ni Umuhimu wa kunyonyesha
maziwa ya mama pekee yake kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo bila
kumpatia mtoto vyakula vya ziada , baada ya kujifungua umuhimu wa
kutumia njia za kisasa za Afya ya UZAZI ili kuzuia kupata mimba nyingine
ndani ya miaka miwili.
Ili
kuruhusu mtoto kukua na kuwa na afya bora , kuhakikisha mama na Mtoto
mchanga analala ndani ya chandarua kilichotiwa dawa ili kujikinga na
ugonjwa wa Malaria, pamoja na umuhimu wa kumpeleka mtoto mchanga katika
kituo cha kutolea huduma za afya mara tu unapogundua dalili za ugonjwa.
Ameongeza
kuwa kupitia mradi wa Tulonge Afya wanawafikia jamiii kupitia njia
mbalimbali ikiwa ni pamoja na uundwaji wa vikundi,elimu kwa njia
mbalimbali lengo likiwa ni kuwafikia walengwa katika makundi yao ili
waweze kuelimika na kufuata kanuni bora za afya kama inavyoelekezwa na
wataalam.
Mratibu
wa uhamasishaji huduma za jamii kutoka ofisi ya mganga mkuu wa manispaa
ya Musoma, Dk. Magreth Shaku aliishukuru asasi hiyo kwa kuamua
kutekeleza mradi huo ndani ya manispaa ya Musoma kwa maelezo kuwa mradi
huo umekuja muda muafaka hivyo utasaidia katika kuongeza uelewa wa jamii
juu ya masula mbalimbali ya afya ikiwemo suala la kunyonyesha watoto
hasa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo mtoto anapozaliwa.
Dk.
Shaku alisema kuwa suala la unyonyeshji wa watoto bado linakabaliwa na
changamoto mbalimbali zinazopelekea akinamama kushindwa alkunyonyesha
kama inavyoshauriwa kitaalam hali ambayo kwa namna moja ama nyingine
imekuwa ikileta changamoto katika suala zima la makuzi ya mtoto.
Alizitaja
baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja na baadhi ya akinamama kukataa
kunyonyesha watoto wao wakidai kuwa maziwa yao yataanguka pamoja na
ushiriki hafifu wa akinababa kwenye suala zima la malezi ya mtoto.
Aliwataka
akinamama kuhakikisha kuwa wananyonyesha watoto ipasavyo kwa maelezo
kuwa mbali na unyonyeshaji kuwa na manufaa katika makuzi ya watoto
lakini pia ni njia kuu mojawapo ya kumkinga mama dhidi ya ugonjwa wa
saratani ya matiti.
Naye
mratibu wa mradi huo, Cyprian Lungu, alisema Mradi wa USAID Tulonge
Afya ni mradi miaka mitano unatekelezwa na serikali kwa kushirikiana na
shirika la FHI360 na wadau wengine chini ya ufadhili wa shirika la
kimarekani lijulikanalo kama USAID. Mradi huu unatekelezwa hapa nchini
katika Wilaya 29 kwenye mikoa 12. Kwa upande wa mkoa wa Mara mradi
unatekelezwa katika wilaya mbili ambazo Musoma Manispaa na Rorya
Aliongeza
kuwa mradi huo unalenga kuleta mabadiliko ya tabia kwa kupambana na
tabia hasi katika jamii zinazouia wanajamii kupata huduma bora za afya.
Alisema
kuwa akinamama watapata elimu juu ya namna wanavyotakiwa kujiandaa
kiafya kabla na baada ya kujifungua pia namna bora ya kuwalea watoto wao
katika umri wa chini ya miaka mitano jambo ambalo litasaidia kuwa na
jamii iliyo bora.






No comments :
Post a Comment