************************************
Baadhi ya Viongozi wa dini walioshiriki
katika kikao Cha siku moja kilichoandaliwa na (NEC )kilichofanyika
Katika Ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha leo.
Na.Woinde Shizza, Arusha
Zikiwa zimesalia siku 29 nchi ya Tanzania iingie kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 wa
kumchagua Rais,wabunge na madiwani,wananchi wametakiwa kuilinda Amani,utulivu pamoja na kufuata taratibu na kanuni za nchiMkurugenzi Mkuu wa uchaguzi Dkt.Charles Mahera
akizungumza na wadau wa Taasisi za kiraia,Viongozi wa dini ,wazee wa
Kimila lna watu wenye mahitaji maalum alisema Tume imejipanga kuwa na
Uchaguzi wenye utulivu wa hali ya juu.
Dkt Mahera alisema kuwa Kati ya wapiga kura
29,188,347 walioandikishwa wanawake ni 14,496,604 ambao ni sawa na
49.67%,vijana wenye umri wa Miaka 18-35 ni 15,650,998
Vijana wa kiume Ni 7,804,845 na wa kike Ni 7,846,153
Aidha kuna jumla ya watu wenye ulemavu
13,211na Kati yao 2,223 Wana ulemavu wa macho ,4,911 Wana ulemavu wa
mikono,6,077 Wana ulemavu wa aina nyingine
Alibainisha kuwa tume hiyo itatumia vituo
vya kupigia kura 80,155 katika zoezi la kupiga kura tarehe 28/9/2020
,Kati ya vituo hivyo Tanzania Bara itakuwa na vituo 79,670 na Tanzania
Zanzibar itakuwa na vituo 685 pia itatumia vituo 1,412 vya NEC kwa
upande wa Zanzibar tume imeridhia mipaka ya majimbo Kama
ilivyorekebishwa na tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, kila kituo Kati ya
hivyo kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500
Aidha aliwataka wadau hao kwenda kutoa Elimu
kwa jamii na kuwaasa kwenda kumsikiliza Sera ili waweze kumchagua
kiongozi wanaompenda
Akichangia Mara katika kikao Askofu wa
Kanisa la Menonite Amos Mhagachi alisema kuwa Ni vyema take makundi
yanayifanya fujo katika kipindi Cha Kampeni wachukuliwe hatua za
kisheria ili Amani iliyopo uendelee kutunzwa.
Attachments area
No comments :
Post a Comment