MFANYABIASHARA
Geofrey Kilimba (47) mkazi wa Salasala kilimahewa jijini Dar es Salaam,
amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi
ya uhujumu uchumi yenye mashtaka manne likiwemo la kukwep kodi na
kuisababishia TRA hasara ya Sh. Milioni 48.8
Akisoma hati ya Mashtaka wakili wa serikali Mkuu Paul Kadushi akisaidiana na wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai katika shtaka la kwanza kuwa, kati ya Agosti 29, 2013 na Agosto 8, 2020 mshtakiwa Kilimba akiwa na wenzake ambao hawapo mahakamani, kwa makusudi walisaidia kutendeka kwa makosa ya uhujumu uchumi akiwa na madhumuni au nia ya kutekeleza kosa la genge la uhalifu.
Imeendelea kudaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Godfrey Isaya kuwa siku hiyo hiyo katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam mshtakiwa alikwepa kulipa kodi ya Sh. Milioni 48.8 ambayo alipaswa kulipa kwa TRA.. Iliyopaswa kulipwa kwa TRA.
Aidha mshtakiwa huyo anadaiwa kuisababishia TRA hasara ya kiasi hicho cha Sh. M.48, 806,922
Katika shtaka la mwisho, mshtakiwa Kilimba anadaiwa kati ya Agosti 29, 2013 na Agosti 8,2020 ndani ya la Darves salaam, alijipatia kiasi hicho cha fedha huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kukwepa kodi na kushiriki genge la uhalifu na makosa mengine ya jijini.

Hata hivyo mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 30, 2020.

No comments :
Post a Comment