Wednesday, September 30, 2020

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII DKT. ALOYCE K. NZUKI AONGOZA KIKAO CHA KUANDAA MKAKATI WA KUENZI NA KUTANGAZA MAISHA YA MWL.NYERERE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa kumuenzi Mwl. Julius Kambarage Nyerere Dkt. Aloyce K. Nzuki (kushoto) akifungua Kikao hicho cha kumuenzi Mwl. Nyerere kilichofanyika kwenye ukumbi wa  TANAPA uliopo kwenye jengo la PSPF Jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Allan Kijazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti  wa Kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa kumuenzi Mwl. Nyerere Dkt. Aloyce K. Nzuki (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Allan Kijazi (wanne kushoto), pamoja na Wajumbe wa Kikao hicho mara baada ya kikao kufanyika kwenye ukumbi wa TANAPA uliopo kwenye jengo la PSPF Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti  Kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa kumuenzi Mwl. Nyerere Dkt. Aloyce K. Nzuki (kulia)  akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Malikale Dkt. Fabian Kigadye wakati wa   Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa  TANAPA uliopo jengo la PSPF Jijini Dododma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti  Kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa kumuenzi Mwl. Nyerere Dkt. Aloyce K. Nzuki (kushoto)  akifafanua mbinu bora za kutumia ili kufanikisha suala la mpango mkakati wa kumuenzi Mwl. Julius Kambarage Nyerere wakati wa Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa  TANAPA uliopo jengo la PSSF Jijini Dododma. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akitoa maoni ya namna bora za kutumia ili kufanikisha mpango  mpango mkakati wa kumuenzi Mwl. Julius Kambarage Nyerere wakati wa Kikao cha kuwasilisha mpango huo kilichofanyika kwenye ukumbi wa  TANAPA uliopo jengo la PSPF Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu, ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Balozi Joseph Sokoine (kulia) kabla ya kuanza kwa Kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa kumuenzi Mwl. Julius Kambarage Nyerere   kilichofanyika kwenye ukumbi wa  TANAPA jengo la PSPF, Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine  akichangia mada wakati wa Kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa kumuenzi Mwl. Julius Kambarage Nyerere kilichofanyika kwenye ukumbi wa TANAPA kwenye Jengo la PSPF, Jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu- Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Firimin Msiangi akifafanua jambo wakati wa Kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa kumuenzi Baba wa Taifa, Mwl.Nyerere kilichofanyika kwenye ukumbi wa TANAPA Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkakati wa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Bw. Imani Kajula akitoa taarifa fupi ya namna ambavyo atatumia mbinu ya kukamilisha mpango mkakati wa kumuenzi Mwl. Nyerere wakati wa Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa TANAPA uliopo kwenye Jengo la PSPF, Jijini Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt.Noel Lwoga akielezea faida za kuendeleza historia ya Mwl, Nyerere kupitia njia mbalimbali wakati wa Kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa kumuenzi Baba wa Taifa kilichofanyika kwenye ukumbi wa TANAPA Jijini Dodoma.

Mtoto wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Godfrey Madaraka Nyerere akitoa maoni wakati wa Kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa kumuenzi Baba wa Taifa, Mwl.Nyerere katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa TANAPA kwenye Jengo la PSPF, Jijini Dodoma.

 

No comments :

Post a Comment