Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya rufaa ya Haydom Mkoani Manyara, Dokta
Paschal Mdoe akisoma taarifa ya gharama za majengo na vifaa tiba vipya
vilivyonunuliwa hivi karibuni
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara, Hudson
Starnley Kamoga akizungumza kwa niaba ya Serikali kwenye uzinduzi wa
majengo na vifaa tiba kwenye hospitali ya rufaa ya Haydom.
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Haydom Mkoani Manyara, wakionyesha namna wanavyotoa huduma kwa watoto.
Askofu
wa Dayosisi ya Mbulu Nicholaus Nzangazelu akizungumza wakati
alipobariki majengo na vifaa tiba vipya vilivyonunuliwa hivi karibuni
vya hospitali ya rufaa ya Haydom.HOSPITALI ya rufaa ya Haydom Mkoani Manyara, imezidi kuboresha
miundombinu yake kwa kuongeza majengo na kununua vifaa tiba vya thamani ya sh1 bilioni hivyo kuzidi kufanikisha kupandishwa hadhi kuwa hospitali ya rufaa ya Kanda.Hospitali
hiyo hutoa huduma kwa wananchi wa wilaya za Babati, Hanang' na Mbulu za
mkoani Manyara, wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Mkalama na Iramba
mkoani Singida, Meatu mkoani Simiyu na Igunga mkoani Tabora.
Kaimu
Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya Haydom, Dk Paschal Mdoe akizungumza
jana kwenye uzinduzi wa majengo na vifaa hivyo alisema hospital hiyo
ina nyota nne za ubora wa huduma na nyota tatu za ubora wa maabara.
Dk
Mdoe alisema jengo la kusafisha figo na mashine saba imejengwa na wadau
wao African health Network na wanasubiria kibali cha Wizara ya Afya ili
ianze kutoa huduma.
Alisema
jengo la maabara (microbiology) wamelikarabati kwa fedha zao za ndani
kwa sehemu na fedha toka serikali ya Norway kupitia shirika la Kikristo
la misaada Norway (NCA).
"Vitanda
20, magodoro 20, makabati 20 na viti matairi saba ukiwa ni msaada wa
rafiki yetu Magna maarufu kama fundi bomba, vya thamani ya sh100
milioni, alivinunua Norway na kuzisafirisha hadi Haydom," alisema Dk
Mdoe.
Alisema
mashine ya kuwapea wagonjwa dawa za nusu kaputi (Anaesthesia mashine)
ya sh45 milioni, mashine ya uchunguzi wa magonjwa ya mfumo wa chakula,
haja kubwa na njia ya hewa (Endoscope) ni msaada wa Profesa Levente
Diosady na Lorne Heuckrof na mkewe Joyce wa Canada.
Alisema
matengenezo na ufungaji wa mashine ya mishipa (Intavenous fluid)
umegharimu sh100 milioni na kufadhiliwa na serikali ya Norway kupitia
NCA na GE Healthcare ya Norway.
Askofu
wa KKKT Dayosisi ya Mbulu, Nicholaus Nsangazelu alisema hospital hiyo
ina zaidi ya miaka 60 katika kutoa huduma kwa jamii.
Askofu
Nsangazelu alitoa wito kwa viongozi wa serikali kuhakikisha
wanafanikisha hospitali hiyo kupandishwa hadhi kuwa hospitali ya rufaa
ngazi ya kanda.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga alisema
serikali imefanikisha kujenga hospitali ya wilaya na vituo vya afya ili
kupunguza msongamano wa wagonjwa hospitali ya Haydom.
Kamoga alisema wataendelea kusukuma mbele hatua ya hospitali ya rufaa ya Haydom kutangazwa kuwa ya rufaa ngazi ya kanda.
Mkazi wa eneo la Haydom, James Gitonge aliipongeza hospitali hiyo kwa namna inavyotoa huduma kwa jamii.
No comments :
Post a Comment