Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya rufaa ya Haydom Mkoani Manyara, Dokta Paschal Mdoe akisoma taarifa ya gharama za majengo na vifaa tiba vipya vilivyonunuliwa hivi karibuni
Askofu wa Dayosisi ya Mbulu Nicholaus Nzangazelu akizungumza wakati alipobariki majengo na vifaa tiba vipya vilivyonunuliwa hivi karibuni vya hospitali ya rufaa ya Haydom.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara, Hudson Starnley Kamoga akizungumza kwa niaba ya Serikali kwenye uzinduzi wa majengo na vifaa tiba kwenye hospitali ya rufaa ya Haydom.
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Haydom Mkoani Manyara, wakionyesha namna wanavyotoa huduma kwa watoto
…………………………………………………………………….
HOSPITALI ya rufaa
ya Haydom Mkoani Manyara, imezidi kuboresha miundombinu yake kwa
kuongeza majengo na kununua vifaa tiba vya thamani ya sh1 bilioni hivyo
kuzidi kufanikisha kupandishwa hadhi kuwa hospitali ya rufaa ya Kanda.
Hospitali hiyo hutoa
huduma kwa wananchi wa wilaya za Babati, Hanang’ na Mbulu za mkoani
Manyara, wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Mkalama na Iramba mkoani
Singida, Meatu mkoani Simiyu na Igunga mkoani Tabora.
Kaimu Mkurugenzi wa
hospitali ya rufaa ya Haydom, Dk Paschal Mdoe akizungumza jana kwenye
uzinduzi wa majengo na vifaa hivyo alisema hospital hiyo ina nyota nne
za ubora wa huduma na nyota tatu za ubora wa maabara.
Dk Mdoe alisema jengo
la kusafisha figo na mashine saba imejengwa na wadau wao African health
Network na wanasubiria kibali cha Wizara ya Afya ili ianze kutoa
huduma.
Alisema jengo la
maabara (microbiology) wamelikarabati kwa fedha zao za ndani kwa sehemu
na fedha toka serikali ya Norway kupitia shirika la Kikristo la misaada
Norway (NCA).
“Vitanda 20, magodoro
20, makabati 20 na viti matairi saba ukiwa ni msaada wa rafiki yetu
Magna maarufu kama fundi bomba, vya thamani ya sh100 milioni, alivinunua
Norway na kuzisafirisha hadi Haydom,” alisema Dk Mdoe.
Alisema mashine ya
kuwapea wagonjwa dawa za nusu kaputi (Anaesthesia mashine) ya sh45
milioni, mashine ya uchunguzi wa magonjwa ya mfumo wa chakula, haja
kubwa na njia ya hewa (Endoscope) ni msaada wa Profesa Levente Diosady
na Lorne Heuckrof na mkewe Joyce wa Canada.
Alisema matengenezo
na ufungaji wa mashine ya mishipa (Intavenous fluid) umegharimu sh100
milioni na kufadhiliwa na serikali ya Norway kupitia NCA na GE
Healthcare ya Norway.
Askofu wa KKKT
Dayosisi ya Mbulu, Nicholaus Nsangazelu alisema hospital hiyo ina zaidi
ya miaka 60 katika kutoa huduma kwa jamii.
Askofu Nsangazelu
alitoa wito kwa viongozi wa serikali kuhakikisha wanafanikisha hospitali
hiyo kupandishwa hadhi kuwa hospitali ya rufaa ngazi ya kanda.
Mkurugenzi mtendaji
wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga alisema serikali
imefanikisha kujenga hospitali ya wilaya na vituo vya afya ili kupunguza
msongamano wa wagonjwa hospitali ya Haydom.
Kamoga alisema wataendelea kusukuma mbele hatua ya hospitali ya rufaa ya Haydom kutangazwa kuwa ya rufaa ngazi ya kanda.
Mkazi wa eneo la Haydom, James Gitonge aliipongeza hospitali hiyo kwa namna inavyotoa huduma kwa jamii.
No comments :
Post a Comment