Bofya Hapa kupata orodha ya FIRST SELECTION
Bofya Hapa kupata orodha ya SECOND SELECTION
BOFYA <<HAPA>> KUONA MAJINA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI, 2020
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa wanafunzi 7,586 kati ya 8,603 walikosa nafasi awamu ya
kwanza wamechaguliwa kijiunga na kidato cha tano katika awamu ya pili.
Akitoa taarifa kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha tano awamu ya pili leo Waziri Jafo amesema kati ya wanafunzi waliochanguliwa ambao ni asilimia 88.18 ya waliokosa nafasi awamu ya kwanza walikuwa wasichana 1,109 na wavulana ni 6,477.
Amesema baada ya kukamilika kuchagua wanafuzi wa kujiunga kidato cha tano awamu ya kwaza, wanafunzi 8,603 wakiwamo wasichana 1,281 na wavulana 7,322 hawakupangiwa shule.
Waziri Jafo amesema wanafunzi 355 ikiwa ni wavulana 254 na wasichana 101 wamebadilishiwa kutoka vyuo mbalimbali na kujiunga na masomo ya kidato cha tano.
Amesema kati ya wanafunzi waliochaguliwa, wanafunzi 615 wamepangiwa tahasusi za sayansi na hisabati na wanafunzi 6,971 wamepangiwa tahasusi za masomo ya sanaa na biashara.
Aidha, Waziri Jafo amesema jumla ya wanafunzi 1,017 wakiwamo wasichana 172 na wavulana 845 sawa na asilimia 11.82 wamekosa tahasusi zinazokidhi vigezo, hivyo kushindwa kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika awamu ya pili.
“Wanafunzi waliokosa nafasi za kujiunga na masomo ya kidato cha tano kwa kukosa tahasusi zinazokidhi vigezo wanashauriwa kuomba nafasi za masomo katika vyuo vinavyosimamiwa na NACTE.” Amesisitiza Waziri Jafo
Aidha Waziri Jafo amewataka wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano awamu ya pili kuhakikisha wanafika shuleni kuanzia Septemba 6 hadi 20 mwaka huu ambapo mwanafunzi atakeyeshindwa atakuwa amepoteza nafasi yake.
No comments :
Post a Comment