*************************************
Leo Septemba 19 , 2020 Zaidi ya wachimbaji wadogo 100 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Geita wamepata mwanga mpya uliojaa matumaini juu ya mbinu mbalimbali za
utafutaji , uchimbaji na Uchenjuaji wa Madini kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).GST kupitia wataalam wake wametoa mwanga mpya kwa wachimbaji wadogo kupitia uwasilishaji wa mada juu ya matumizi ya mbinu za kisasa za utafuta madini.
GST kupitia wataalam wake imetoa mada husika katika njia mbalimbali ikiwemo namna Bora ya Utafutaji , Uchimbaji na Uchenjuaji wa Madini.
Sambamba na semina hii GST ilipata fursa ya kutembelewa na wachimba wadogo wakiwa na hamu ya kuona vifaa vya Utafiti wa madini pamoja na kufahamu jinsi taarifa za Jiolojia zinavyochakatwa.
Akiongea na GST mapema baada ya semina kuisha mchimbaji mdogo ambaye pia ni mwanachama Cha wachimbaji wadogo mkoani Geita GEREMA Mariam Kome aliishukuru GST kwa kutoa mwanga mpya hususani katika Uchenjuaji wa Madini.
Naye mchimbaji mdogo kutoka Mwanza James alisema semina hii italeta tija katika Utafutaji wake , uchimbaji kwani kwa mara nyingi amekuwa akichimba bila kujua namna za uchimbaji Ila kupitia semina hii nimepata mwanga.
Semina hii ya siku tatu imeisha Leo huku wachimbaji wakiendelea kupata Elimu kupitia maonesho ya vitu mbalimbali.
No comments :
Post a Comment