Afisa
Mkuu wa Huduma Shirikishi wa Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli akizungumza
katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki hiyo kwenye
hoteli ya Gran Melia jijini Arusha.
NMB
ilitangaza unafuu wa ulipaji mikopo kwa wateja wake mwezi Mei mwaka
huu, kupitia likizo ya marejesho ya mikopo yao na wengine wakiongezewa
muda wa kulipa mikopo hiyo ili kuwasaidia kukabiliana na madhara
yaliyoletwa na COVID–19 katika biashara zao.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Longido - Frank Mwaisumbe
alisema NMB iliwasaidia sana wateja wake na imeendelea kuwa nao karibu
wakati wote wa kipindi cha COVID-19 na wao kama Serikali wanawapongeza
kwa hilo. Ni jambo kubwa hasa kwa Sekta ya Utalii ambayo imeathiriwa
sana na COVID-19. Siyo hivyo tu, Frank vilevile aliipongeza Benki hiyo
kwa utaratibu wake wa kukutana na wateja jambo ambalo alisema linasaidia
kuboresha mahusinao kati ya Benki na wateja wao.
Wafanyabiashara
wakubwa ambao ni wateja wa Benki ya NMB mikoa ya Arusha na Kilimanjaro
wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki hiyo
kwenye hoteli ya Gran Melia jijini Arusha kujadili mikakati ya
kuboresha ushirikiano .
Naye
Afisa Mkuu wa Huduma Jumuishi wa NMB - Nenyuata Mejooli alisema, Benki
ya NMB ilitoa ahuweni kwa wateja wake ili kuhakikisha shughuli zao
zinastahimili misukosuko ya COVID-19 ikiwemo kubadilisha mfumo wa
urudishaji mikopo kulingana na ukubwa wa athari.
Wakati
huohuo, Nenyuata, aliwapongeza wateja wao kwa ukakamavu waliouonyesha
kipindi cha COVID-19 na kuahidi kuendelea kuwa nao bega kwa bega.
“Tunaelewa katika kipindi hiki,biashara kama utalii na sekta ya hoteli
zilipata changamoto. Sisi kama NMB tumehakikisha tupo karibu zaidi nanyi
wateja wetu ili kuhimili changamoto hizo zilizojitokeza,” aliongeza.
Wiki
hiyohiyo, NMB pia iliweza kuwakutanisha wateja wadogo na wa kati
walioujiunga na mtandao maalumu wa ‘NMB Business Club’ na kuwapa elimu
ya masuala ya kibenki ikiwemo mifumo mipya ya malipo kupitia NMB
Mkononi, Mastarcard QR pamoja na huduma zingine za Benki kama Bima (NMB
Bancassuarance).
Tangu
kuanzishwa kwa NMB Business Club miaka sita iliyopita, mtandao huo upo
kwenye Mikoa ya; Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Mtwara,
Mbeya na Dodoma huku washirika wake wakiwa zaidi ya 600.
Washiriki
wa kongamano la wafanyabiasha Wadogo na wa Kati waliojiunga na Mtandao
wa NMB Business Club kutoka Arusha, Moshi na Tanga wakiwa katika
kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.
Mwakilishi
wa kiwanda cha ngozi cha Tanneries kutoka Himo Wilaya ya Moshi - France
Sawerio kulia,akitoa maelezeo kwenye maonesho ya bidhaa anazo
zitengeneza,wakati Viongozi wa Benki ya NMB walipo tembelea banda lake
wakati wa Kongamano la wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (NMB Business
Club), lililofanyika katika ukumbi wa Kuringe - mjini Moshi.
Serikali na wadau mbalimbali wameipogeza Benki ya NMB kwa msaada wake
mkubwa wakulisaidia Taifa na wateja wake kukabiliana na changamoto za janga la COVID-19 ambalo athari zake kiuchumi na kibiashara zinaendelea kuitikisa dunia.
No comments :
Post a Comment