Kushoto ni Afisa Masoko wa Kampuni ya ETC Agro, John Joseph na Meneja
wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui wakimkabidhi Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko mfano wa funguo ya trekta
wakati wa uzinduzi wa za huduma ya mikopo ya zana za kilimo uliofanyika katika benki ya CRDB tawi la Shinyanga leo Jumanne Septemba 22,2020. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui, kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB, Luther Mneney. Wa pili kulia Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa Uzinduzi wa huduma ya Mikopo ya zana za kilimo kutoka Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya kilimo ‘ETC Agro,Agricom na Loan Agro
Meneja
wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akiwakaribisha wakulima
binafsi,kutoka kwenye vikundi kukopa zana za kilimo kwani hakuna
masharti magumu kama dhamana.
Muonekano wa sehemu ya Matrekta ambayo wakulima wanaweza kukopa
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mikopo ya zana za kilimo. Kushoto ni Afisa
Masoko wa Kampuni ya ETC Agro, John Joseph. Wa kwanza kulia ni Meneja
wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akifuatiwa na Meneja wa
Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akijaribu kuendesha trekta wakati wa uzinduzi wa mikopo ya zana za kilimo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) na Meneja
wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui wakifurahia jambo baada
ya kupanda kwenye matrekta wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo ya
Zana za Kilimo.Katikati ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga,
Luther Mneney.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi funguo ya Trekta
Mkulima kutoka Bariadi mkoani Simiyu Malugu Masanja Nshashi (kushoto)
aliyenunua trekta kwa njia ya mkopo kupitia Benki ya CRDB.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi funguo ya Trekta Mkulima kutoka Bariadi mkoani Simiyu Manjobola Mome (kulia) aliyenunua trekta kwa njia ya mkopo kupitia Benki ya CRDB.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi funguo ya Trekta Mkulima kutoka Bariadi mkoani Simiyu Manjobola Mome (kulia) aliyenunua trekta kwa njia ya mkopo kupitia Benki ya CRDB.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya
kumbukumbu na viongozi wa benki ya CRDB, Kampuni ya ETG Agro na wakulima
kutoka Bariadi mkoani Simiyu walionunua matrekta kwa njia ya mkopo.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Benki
ya CRDB Kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya
kilimo ‘ETC Agro,Agricom na Loan Agro wamezindua huduma ya Mikopo ya
zana za kilimo yakiwemo matrekta kwa wakulima ili kuwawezesha kukopa kwa
riba nafuu bila kuweka dhamana ya ziada ili kuboresha kilimo chao.
Uzinduzi wa Mikopo ya zana za kilimo umefanyika leo Jumanne
Septemba 22,2020 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga ambapo Mgeni
rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa mikopo ya zana za
kilimo, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko aliipongeza
Benki ya CRDB kwa ubunifu wao wa mara kwa mara katika kurahisisha
uboreshaji wa maisha ya Watanzania kiuchumi na hasa katika kuunga mkono
juhudi za serikali kuondoa umaskini wa kipato kwa wananchi wake.
“Benki ya CRDB mmetia fora katika sekta ya kilimo,wakati
wa msimu wa pamba napo mlishiriki kikamilifu kutoa fedha na leo mmekuja
na mikopo ya zana za kilimo,yakiwemo matrekta haya tena bila dhamana za
ziada”,alisema.
Mboneko alieleza kuwa matrekta hayo yatawasaidia wakulima
kuboresha kilimo chao badala ya kutumia jembe la mkono na majembe ya
kukokotwa na ng’ombe ili kuongeza uzalishaji hivyo kilimo kuwa na tija
zaidi.
“Naomba wakulima mchangamkie fursa ya kununua matrekta
yaliyotolewa na Benki ya CRDB kupiti wadau ambao ni ETC Agro (wauzaji wa
matrekta ya Mahindra), Agricom (wauzaji wa matrekta ya Swaraj na
Kubota) na Loan Agro (wauzaji wa matrekta ta John Deer)”,alisema Mboneko.
“Hongereni sana Benki ya CRDB,Mara zote CRDB mmekuwa
wabunifu wa kushiriki kwa karibu katika miradi mbalimbali ya kimkakati
ya serikali yetu hasa kwa kipindi hiki ambacho Tanzania ipo katika
uchumi wa kati”,aliongeza Mboneko.
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wakulima,vyama vya msingi vya
mazao (AMCOS),wakulima binafsi hususani wa zao la pamba,mpunga na
alizeti kuchangamkia fursa ya mikopo ya zana za kilimo ili kuhakikisha
kilimo chao kiwe na tija zaidi.
Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya
Magharibi, Said Pamui alisema benki ya CRDB kwa kushirikia na Makampuni
ya uuzaji matrekta ‘ETC Agro,Agricom na Loan Agro’ wameboresha taratibu
za utoaji wa mikopo ya zana za kilimo kupitiaa benki ya CRDB ili
kuwawezesha wakulima kukopa bila kuweka dhamana ya ziada kwa riba nafuu.
Alieleza kuwa benki ya CRDB imeamua kuleta wadau wa
maendeleo ya kilimo ili kuwapunguzia wakulima riba kubwa na kupata
mikopo ya dhana za kilimo bila kutumia hati za nyumba ambapo pia
matrekta yatakuwa yanafanyiwa matengenezo na wauzaji hao wa matrekta.
“Benki ya CRDB ni benki ya Kimkakati inayounga mkono
jitihada za serikali kuwaongezea kipato wananchi na imekuwa
ikishirikiana na serikali bega kwa bega kutekeleza miradi ya kuwaletea
maendeleo wananchi na imechangia nchi kufikia uchumi wa kati”,alisema Pamui.
Aidha alisema benki ya CRDB, ni benki ya wananchi na
inaongoza kuwa karibu wakulima na kwamba hatarajii kuona wakulima
wanaendelea kulima kizamani kwa kutumia majembe ya mikono ama ya
kukokotwa na ng’ombe.
Naye Afisa Masoko wa Kampuni ya ETC Agro, John Joseph
alisema kupitia mikopo ya zana za kilimo,kinachotakiwa kufanywa na
wakulima ni kutoa mchango wao katika ununuzi wa trekta usiopungua 25% ya
bei ya trekta.
Katika uzinduzi huo wa huduma ya mikopo
ya zana za kilimo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko
amekabidhi matrekta kwa wakulima wawili kutoka Bariadi mkoani Simiyu
ambao ni Njobola Ng’weleja Mome na Malugu Masanja Shashi.
No comments :
Post a Comment