Monday, August 17, 2020

WAZIRI WA UWEKEZAJI ATEMBELEA AIRTEL TANZANIA

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angela Kairuki lakifuatilia kwa makini maelezo ya watendaji Mkuu wa Airtel nchini leo alipofanya ziara maalum Katika ofisi kuu ya Airtel iliyopo jijini Dar es salaam.Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel akiongea na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angela Kairuki kufanya  ziara maalum Katika ofisi kuu ya Airtel jijini Dar es salaam na kukutana na uongozi wa Airtel akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw, George Mathen.

***************************

WAZIRI WA UWEKEZAJI ATEMBELEA AIRTEL TANZANIA Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angela Kairuki leo amefanya ziara maalum Katika ofisi kuu ya Airtel iliyopo

jijini Dar es salaam na kukutana na uongozi wa Airtel akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw, George Mathen.

Mheshimiwa waziri amesema ziara hiyo ni sehemu ya majukumu yake ambapo lengo  ni kupitia maendeleo na kupokea moja kwa moja baadhi ya changamoto wanazopitia wawekezaji wanahudumiwa na wizara yake ili kuzipatia suluhisho Airtel ikiwa ni  sehemu ya uwekezaji nchni,  serekali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania inamiliki kampuni hiyo kwa 49% huku 51% ni uwekezaji wa mbia Bhrati Airtel. 

Mheshimiwa Waziri Kairuki amesema serikali inaendeleza ushirikiano na bora wawekezaji nchini ili pande zote ziweze kufaidika na uwekezaji wowote.

Nae Mkurugenzi Mkuu airtel Bw George Mathen amesema kampuni yake itaendelea kutoa mawasiliano yenye tija nchni pamoja na  kuhakikisha inalipa kodi kwa mujibu wa sheria.

Bwana Mathen alisema “Airtel tutaendelea kushirikiana na serikali kutoa huduma bora ya mawasiliano kama ilivyo makubaliano yetu na serikali ikiwa ni pamoja na kuliapa kodi”

Mbali na kuboresha mawasiliano Bw, Mathen alieleza kuwa Airtel itaendelea kujihusisha na  miradi yake ya  kusaidia jamii kama  Airtel FURSA ili kusaidia vijana nchni kama inavyofanya na VETA kupita mradi wa  VSOMO, Airtel Fursa Lab pamoja na mradi wa redio za jamii (community Redio) unaofanywa na Airtel kwa Kushirikiana na UNESCO

 

No comments :

Post a Comment