Sunday, August 2, 2020

WAZIRI MPINA ATAKA MAONYESHO YA 88 KUTUMIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAKULIMA,WAVUVI NA WAFUGAJI



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akikagua zana za Kilimo katika Banda la Farmbase ilipotelea maonesho ya wakulima nanenane kanda ya ma shariki katika viwanja vya Mwalim Julius Nyerere Manispaa ya Morogoro
Muonekano wa Banda la wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kanda ya mashariki.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akiangalia viatu vilivyotengezwa kwa ngozi katika banda la wizara ya mifugo mkoani Morogoro ambapo yanafanyika maonesho ya wakulima nanenae kanda ya mashariki.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akiangalia vitalu vya mazao ya mbogamboga yanayozarishwa na kampuni ya Balton
……………………………………………………………………………
NA FARIDA SAIDY,MOROGORIO.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina ametembelea maonesho ya wakulima nanenane kanda ya
mashiriki inayoundwa na Mikoa Nne ya Pwaani,Tanga Morogoro na Dar es salaam na kuonesha kulidhishwa na kazi kubwa zinazofanywa na waandaaji wa maeonesho hayo.
Akizungumza mara baada ya kujionea kazi zinazofanywa katika maonesho hayo Waziri Mpina amesema Mwaka huu washiriki wametumia ubunifu mkubwa ambao utaleta tija katika uzarishaji kwa wakulima,wavivi na wafugaji watakaotembelea maonesho hayo.
Aidha amezitaka Taasisi na Mashirika yanayoshiriki katika maonesho ya wakulima nanenane kuwa na takwimu pamoja na taarifa zote sahihi zinazohusika katika mabanda yao bila ya kuweka mipaka ya kikanda ili kuweza kujibu hoja zinazoibuliwa na wadau wanaotembelea maonesho hayo.
Akiwa katika banda la wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS waziri mpina ameitaka TFS kushikisha wananchi wakati wa kuweka mipaka ili kupunguza Migogoro ya Ardhi,huku Afisa habari wa TFS kanda ya mashariki Suleimani Burenda akisema wamejipanga katika kuzarisha asali na kulinda misitu iliyopo isihalibiwe na wanchi.

No comments :

Post a Comment