Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga akionyesha Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi mwaka 2020 wakati akizungumza kwenye kikao cha dharula na
Menejimenti na watendaji wakuu wa Bodi za mazao pamoja na Taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika Jijini Dodoma Leo tarehe 31
Agosti 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal Wizara ya Kilimo)
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye
kikao cha dharula na Menejimenti na watendaji wakuu wa Bodi za mazao
pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika Jijini
Dodoma Leo tarehe 31 Agosti 2020.
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga akionyesha Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi mwaka 2020 wakati akizungumza kwenye kikao cha dharula na
Menejimenti na watendaji wakuu wa Bodi za mazao pamoja na Taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika Jijini Dodoma Leo tarehe 31
Agosti 2020.
Sehemu
ya watumishi wa Wizara ya Kilimo wakifatilia kikao kazi cha Waziri wa
Kilimo Japhet Hasunga wakati akizungumza kwenye kikao cha dharula na
Menejimenti na watendaji wakuu wa Bodi za mazao pamoja na Taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika Jijini Dodoma Leo tarehe 31
Agosti 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Watumishi
wa Wizara ya Kilimo wameagizwa kuisoma ilani ya Chama Cha Mapinduzi
iliyotolewa na Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Agosti 2020 kwa
ajili ya
uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye
kikao cha dharula na Menejimenti na watendaji wakuu wa Bodi za mazao
pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika Jijini
Dodoma Leo tarehe 31 Agosti 2020.
Waziri
Hasunga amesema kuwa Ilani ya CCM ina mambo mengi makubwa na muhimu ya
kuhusu sekta ya kilimo ambayo yameainishwa katika ukurasa wa 33 mpaka
ukurasa wa 46.
Maeneo
hayo ambayo CCM imebainisha ili serikali yake itakapopewa dhamana kwa
mara nyingine iyatekeleze ni pamoja na usimamizi madhubuti wa Programu
ya kuendeleza sekta ya kilimo Awwamu ya Pili (ASDP II) kwa kusimamia kwa
weledi matumizi bora ya ardhi pamoja na maji ili kuwa na kilimo chenye
tija.
Kuongeza
uzalishaji wa mbegu bora za kilimo, Usimaizi madhubuti wa mbolea na
viuatilifu ili kuondokana na changamoto ya viuatilifu na mbolea feki
kadhalika kuhusu umuhimu wa kuongeza maeneo ya umwagiliaji ikiwa ni
pamoja na usimamizi madhubuti wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji nchini ili
kuondokana na dhana ya kutegemea kilimo cha msimu badala yake kuhamia
katika kilimo cha Umwagiliaji, Tija na kuongeza uzalishaji.
Katika
kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg
Gerald Kusaya na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo,
Waziri Hasunga amemuagiza kila mtumishi wa serikali katika Wizara ya
Kilimo kuitafuta na kuisoma ilani ya uchaguzi ili kutafakari na
kujiandaa kwa ajili ya utekelezaji wake kwani imani yake CCM itashinda
kwa kishindo na hivyo kuendelea kuongoza dola.
Amesema kuwa katika ukurasa wa juu wa ilani uliopambwa na kauli mbiu isemayo “Tumetekeleza kwa Kishindo, Tunasonga mbele Pamoja” ilani
inaonyesha dira na muelekeo wa utendaji wa shughuli mbalimbali za
wizara ya kilimo ambapo miongoni mwa picha kumi zilizowekwa juu ni picha
mbili zinahusu sekta ya kilimo hivyo ilani ya CCM imeonyesha umuhimu wa
sekta ya kilimo nchini.
Ilani
hiyo yenye kurasa 303 katika ukurasa wa 30 mpaka 33 imebainisha umuhimu
wa usimamizi wa sekta ya Ushirika ikiwemo kusimamia masoko ya wakulima
kadhalika kuongeza tija ya usiamamizi wa vyama vya Ushirika nchini ili
kuwanufaisha wakulima nchini.
No comments :
Post a Comment