Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia uwekezaji Angellah
Kairuki (wapili kushoto), akifuatana na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet
Hasunga (wa kwanza kushoto), akizungumza jambo wakati alipotembelea
banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kwenye viwanja vya
Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu jana. Wapili Kulia ni Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence akiwa na Afisa kutoka ofisi
ya utawala Neema Mushi.
Afisa kutoka ofisi ya utawala WCF, Neema Mushi.
Wananchi wakipata maelezo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi kwenye banda la WCF viwanja vya Nyakabindi.
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence (kulia), akimfafanulia
jambo mfanyakazi huyu aliyetembelea banda la WCF viwanja vya Nyakabindi
mkoani Simiyu Agosti 3, 2020.
Na mwandishi wetu, Simiyu.
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki
ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kutokana na huduma
ambazo imekuwa ikitoa kwa wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki
kutokana na kazi.
Waziri
Kairuki ametoa pongezi hizo jana (leo Agosti 3, 2020) wakati
alipotembelea katika banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya Nanenane
yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa
Bariadi mkoani Simiyu.
Waziri
Kairuki alitoa pongezi hizo baada ya kupata maelezo ya shughuli za
Mfuko yaliyokuwa yakitolewa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo,
Sebera Fulgence ambapo
Waziri alivutiwa na majibu ya namna fidia inavyolipwa kwa mfanyakazi aliyeumia au kufariki kutokana na kazi.
Waziri alivutiwa na majibu ya namna fidia inavyolipwa kwa mfanyakazi aliyeumia au kufariki kutokana na kazi.
“Mwisho wa siku mtu amepata ulemavu wa kudumu angalau consolation
(faraja) anayopata ni kuona wanae wanaendelea vizuri au kama amefariki
walau fidia isaidie watoto na mjane pia, lengo la serikali ni ku- support for real, ninawapongeza
sana kwa kazi nzuri mnayofanya.” Alisema Waziri Kairuki ambaye alikuwa amefuatana na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga.
sana kwa kazi nzuri mnayofanya.” Alisema Waziri Kairuki ambaye alikuwa amefuatana na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga.
Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi unashiriki katika maonesho hayo ili kukutana
na wadau wote na wananchi kwa ujumla wakiwemo wafanyakazi kutoka sekta
ya Umma na Binafsi
Kauli
mbiu ya mwaka huu ya maonesho hayo yanayofanyika mkoani Simiyu kwa
mwaka wa tatu mfululizo ni “Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua
Viongozi Bora 2020.”.
No comments :
Post a Comment