“Sasa wateja kununua tiketi #ZanFastFerriess kirahisi zaidi kwa #TigoPesa mahali
popote walipo.Tunawashauri wateja wetu kutumia huduma hii ili kuokoa
muda na kulipa kwa urahisi zaidi.” Angelica Pesha-Kaimu Mkuu wa Huduma
za Kifedha wa Tigo Pesa.
|
Wateja wa Tigo kununua tiketi za ZanFast Ferriess kwa Tigo Pesa: Tigo yaingia makubaliano na Kampuni ya usafirishaji ya Vigor Group inayomiliki boti za ZanFast Ferries ili kuwawezesha wateja wake kununua tiketi kwa njia ya #TigoPesa, lengo ni kuboresha huduma za ukataji tiketi kwa wateja wao. |
Kampuni inayoongoza katika kuhakikisha mtanzania anaishi maisha ya kidigitali,Tigo,leo imeingia katika makubaliano na Kampuni
ya usafirishaji ya Vigor Group ambayo inamiliki boti za ZanFast Ferries
ili kuwawezesha wateja wake kununua tiketi kwa njia ya Tigo Pesa, hatua
itakayoboresha huduma za ukataji tiketi kwa wateja wao.
Kampuni
ya ZanFast Ferries ni moja ya watoa huduma za usafiri wa majini kati ya
Zanzibar na Dar es Salaam zinazochangia katika urahisishaji wa huduma
za usafiri kwa wenyeji na wageni.
Kaimu
Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema “Tukiwa
kama kampuni inayoongoza katika huduma za kidigitali Tanzania,tunafuraha
kwa hatua hii kwani inaongeza thamani katika huduma zetu.Kwa sasa
wateja wanaweza kununua tiketi kirahisi zaidi kwa Tigo Pesa mahali
popote walipo.Tunawashauri wateja wetu kutumia huduma hii ili kuokoa
muda na kulipa kwa urahisi zaidi,” alisema Pesha.
Ili
kupata tiketi, mteja wa Tigo atatakiwa kupakua application ya ZanFast
Ferries kisha nenda kata tiketi,chagua Tigo Pesa na fanya malipo.Baada
ya kukamilisha malipo mteja atapokea ujumbe mfupi (SMS) pamoja na
tiketi laini (e-ticket) itakayotumika siku ya safari.
“Tunaamini
njia hii ni suluhu ya muda mrefu na itaboresha namna wateja wanavyopata
huduma za usafiri hususan wasafiri wa ndani kwani kwa sasa hakuna haja
ya kwenda tena katika ofisi bali ukiwa na simu yako tu unaweza
kujihakikishai uhakika wa kupata usafiri,” alisema Pesha.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Vigor Group, Toufiq Turky alieleza
kufarijika na ushirikiano baina yao na Tigo Pesa kwani huduma ya Tigo
Pesa ni huduma ya uhakika na rahisi kutumika mahali popote na kwamba
itarahisisha upatikanaji wa huduma za usafiri kwa wateja wake.
“Ushirikiano baina yetu na Tigo Pesa umetanua wigo wa njia za malipo sanjari na App yetu ya ZanFast Ferries ambazo zinampa mteja uhuru wa kununua tiketi mahali popote alipo,” alisema Turky.
Aliongeza
kuwa kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na Tigo katika kuleta huduma
na bidhaa za kidigitali ili kurahisisha malipo kwa wateja wake.
Wateja
watakaofanya malipo kwa Tigo Pesa watatumia tiketi laini (e-ticket)
badala ya tiketi za kawaida na watatakiwa kuwa nayo siku ya safari.
No comments :
Post a Comment