Waziri wa Kilimo Mh.Japhet Hasunga akitembelea moja ya shamba la mfano wa Shahiri wakati wa maonyesho hayo
…………………………………………………………………………………….
Katika mkakati
wake wa kuwainua wakulima nchini, kampuni ya Tanzania Breweries Public
Limited imewezesha wakulima wa zao la Shahiri kanda ya
kaskazini
inaoshirikiana nao kuhudhuria maonyesho ya kilimo yaliyoandaliwa na
taasisi ya Tanzania Agricultural Research Institute, (TARI na kufanyika
mkoani Arusha.
Kwa kipindi kirefu
kampuni imekuwa ikishirikiana na wakulima wa zao la shahiri kwa
kuwawezesha kuongeza uzalishaji kwa kuwapatia mbegu bora zinazofaa
katika hali ya hewa ya eneo hilo sambamba na kuwahakikishia soko la
uhakika wa mavuno yao.
Meneja Masoko wa
TBL Plc Joel Msechu,alisema kampuni imedhamini wakulima wapatao 100
kuhudhuria katika maonyesho hayo kwa ajili ya kujifunza mbinu za kilimo
cha kisasa na matumizi ya teknolojia katika kuleta mapinduzi ya kilimo
ili ziwasaidia kuongeza uzalishaji.
“Kwetu TBL
tunaamini ushirikiano unaweza kuchochea kuleta maendeleo
endelevu.Maonyesho ya kilimo ni moja ya fursa ya kuwakutanisha wakulima
wetu wa zao la Shahiri na mtama na kuwawezesha kupata maarifa ya
kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika kazi yao”,alisema
Msechu.
Kampuni ya TBL
imedhamiria kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania ya kuleta
mapinduzi ya viwanda kupitia kuwekeza pia katika sekta ya kilimo kupitia
mpango wake wa kushirikiana na wakulima 6,000 wa zao la Shahiri katika
maeneo ya Kilimanjaro,Manyara,Arusha,Iringa na Madaba sambamba na
kujenga kiwanda cha kusindika kimea mkoani Dodoma ambacho kitakuwa na
uwezo wa kuzalisha tani 32,000 za kimea.Kwa sasa kampuni inanua asilimia
74% ya malighafi zake nchini na imedhamiria kuongeza zaidi matumizi ya
malighafi kutoka nchini katika miaka ijayo.
No comments :
Post a Comment