Eng.Mwanji
Y Mhaka, Mhandisi mradi wa umeme wa maji Julius Nyerere (JNHPP-2115)
akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kwenye banda la TANESCO kwenye
maonesho ya Nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi
mkoani Simiyu Agosti 2, 2020.
Elimu
kuhusu matumizi bora ya umeme ikitolewa na mtaalamu huyu wa TANESCO kwa
wakazi wa mji wa Bariadi mkoani Simiyu waliofika katika banda la Shirika
hilo
Wahudumu
wa TANESCO wakiwahudumia wananchi waliofika kwenye banda la shirika
hilo katika maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya
mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Wahudumu
wa TANESCO wakiwahudumia wananchi waliofika kwenye banda la shirika
hilo katika maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya
mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Meneja
wa TANESCO mkoa wa Simiyu, Eng. Khadija Abdallahmed(Watano kushoto),
akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wafanyakazi wa TANESCO katika
banda la shirika hilo
Wakubwa kwa watoto wakielimishwa kuhusu madhara yanayoweza kutokea endapo mtu atashika waya wa umeme uliokatika
NA MWANDISHI WETU, NYAKABINDI
Shirika
la umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kuwahimiza wananchi wote
wakiwemo,... wakulima, wafugaji na wavuvi kutumia fursa za uwepo wa umeme
wa kutosha na wa uhakika ili kujiletea maendeleo.
Hayo
yamesemwa Agosti 2, 2020 na Meneja wa TANESCO mkoa wa Simiyu, Eng.
Khadija Abdallahmed kwenye banda la TANESCO katika maonesho ya Nanenane
yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa
Bariadi mkoani Simiyu.
“Naomba
kutoa wito kwa watanzania wote kwa ujumla wachangamkie hizi fursa za
umeme na maendeleo ya kilimo, mifugo na uvuvi Tanzania nzima, umeme upo
wa kutosha Tanzania nzima, TANESCO tupo tunaaangaza maisha.” Alisisitiza
Eng. Khadija
Alisema
TANESCO inashiriki maonyesho haya kwa vile wao ni wadau wakubwa wa
shughuli za kilimo, mifugo pamoja na uvuvi na kwa huduma ya umeme
itolewayo na shirika hilo ni sehemu ya kufanikisha maonesho hayo.
Aliwakaribisha
wananchi wote wanaopata fursa ya kufika kwenye viwanja vya Nyakabindi
yanakofanyika maonesho hayo kutembeela katika banda la TANESCO kwani
watafaidika na kupata elimu kuhusu matumizi bora na sahihi ya umeme.
“Lakini
wananchi watakaofika kwenye banda letu watakutana na mtaalamu mbobezi
ambaye atawaeleza kuhusu mradi mkubwaj wa kimkakati wa ujenzi wa bwawa
la kufua umeme Julius Nyerere (JNHPP 2115) kwenye bonde la mto Rufiji.”
Alisema.
No comments :
Post a Comment