Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Antony
Mtaka (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM) Prof. Tadeo Satta, alipowasili katika Banda la Wizara ya Fedha na
Mipango, katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika
Viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Antony
Mtaka (wa pili kulia) akiuliza maswali mbalimbli kuhusu miradi ya Ubia
kati ya Sekta Binafsi na Umma, wa kwanza kulia ni Mkuu wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Tadeo Satta, wa tatu kulia ni Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny
Mwaipaja, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango,
katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya
Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Antony
Mtaka (kulia), akieleza jambo kuhusu Mipango ya Kitaifa alipotembelea
dawati la Mipango ya Kitaifa, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya
Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa
katika Viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa
Fedha (IFM) Prof. Tadeo Satta (kulia) akisikiliza ushauri kuhusu Vyuo
kusaidia usimamizi wa maandiko ya miradi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Antony Mtaka (kushoto), alipotembelea Banda la Wizara ya
Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa
katika Viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony
Mtaka (wa nane kulia), Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof.
Tadeo Satta (wa tisa kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja (wa saba kuli), wakiwa
katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Fedha, baada ya
kutembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Nanenane
yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
………………………………………………………………………..
Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Antony Mtaka, ameiomba Wizara ya Fedha na Mipango kutoa
msamaha wa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa mafuta ya kupikia
yanayozalishwa hapa nchini ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo na
tija kwa wenye viwanda.
Bw. Mtaka amsema
kuwa hivi sasa Serikali imeondoa kodi kwenye mbegu za Mafuta jambo
ambalo ni zuri lakini hatua hiyo ingekuwa na tija zaidi endapo kodi hiyo
pia ingepunguzwa au kuondolewa kabisa kwenye Mafuta yanayozalishwa ili
bei ya bidhaa hiyo iweze kupungua na kuchochea uzalishaji wa malighafi
za kuzalisha Mafuta.
Hayo aliyasema
alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa yanayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Alisema kuwa
Tanzania inaagiza Mafuta ya kupikia kwa kiasi kikubwa kutoka nje ya nchi
hivyo msamaha wa VAT katika Mafuta hayo utasaidia kukuza uzalishaji,
ushindani na kuokoa fedha zinazotumika kuagiza Mafuta hayo kutoka nje ya
nchi.
“Kwenye pamba
tunahamasisha kuongeza thamani, pamba izalishe nyuzi na mbegu izalishe
Mafuta na tupate mashudu, sasa mbegu unaisamehe lakini Mafuta unatoza,
bado tunatumia gharama kubwa sana kuingiza Mafuta toka nje”, alieleza
Bw. Mataka.
Aidha kwa upande
wa Taasisi ya Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (UTT- AMIS), alisema kuwa
kiwango cha Serikali kuhamasisha watu kununua hisa za taasisi hiyo iko
chini na kuushauri uongozi wa Taasisi hiyo kutumia fursa ya wafanyakazi
wastaafu hususan walimu ambao wanahitaji kuelimishwa ili washiriki
katika ununuzi wa hisa za Serikali.
Alisema kuwa
wastaafu wanapata changamoto kubwa hasa wanapoingia kwenye sekta binafsi
na kujihusisha na ufugaji na biashara ya vyombo vya moto, baada ya
mwaka mmoja wanafilisika ilihali kuna mahali ambapo angewekeza asilimia
60 ya mafao yake, angepata mshahara uleule kupitia hisa ambazo zingempa
nafasi ya kukopa na kupata gawio kila mwezi.
Bw. Mtaka alisema
kuwa katika ngazi ya Halmashauri, makundi ambayo Serikali inayagusa
kama wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, taasisi za Wizara ya Fedha
na Mipango zina nafasi kubwa ya kutoa ushauri wa namna ya kujitegemea,
kwa kuwa kiasi cha asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri kinachopelekwa
katika makundi hayo tija yake bado ni ndogo.
Kwa upande wake
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga, alisema kuwa Mifumo
ya fedha iliyotengenezwa na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango,
inaisaidia Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kusimamia mapato kwa kuwa
hali halisi ya ukusanyaji inaonekana hivyo kufanya wadau katika ngazi
zote kufanya maamuzi sahihi ya matumizi yake na kuboresha vyanzo vya
mapato.
Aidha Kodi 114 za
sekta ya Kilimo na Mifugo zilizofutwa na Serikali zinachochea ongezeko
la uzalishaji na kuwa na manufaa kwa wakulima katika kuongeza kipato na
makusanyo kwa kuwa uzalishaji utaimarika.
Naye aliyekuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Bw. Jumanne Sajin, ameipongeza Wizara
ya Fedha na Mipango kwa kuwaleta watumishi mahili kutoa elimu kuhusu
masuala ya fedha, mifumo ya fedha, bajeti, Sera, Pensheni, mipango ya
KItaifa, Ubia kati ya Umma na Sekta Binafsi pamoja na taasisi zake
zilizo chini ya Wizara kwa kuwa elimu inayotolewa itachangia wananchi
kuelewa kazi kubwa iliyofanywa na Serikali katika Nyanja mbalimbali.
Maonesho ya
Nanenane yanayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu yapo katika Siku ya tano na
yanatarajia kumalizika Agosti 10 baada ya Waziri mwenye Dhamana ya
Kilimo kuongeza siku mbili ili kutoa fursa kwa wananchi wengi zaidi
kushiriki na kujifunza.
No comments :
Post a Comment