Sunday, August 16, 2020

LUGHA DHALILISHI,RUSHWA YA NGONO, FEDHA NI KIZUIZI CHA WANAWAKE KUGOMBEA UONGOZI


Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa Rose Reuben(Aliyevaa suti nyeusi)

Na.Vero Ignatus.

Lugha dhalilishi,Rushwa ya ngono,Rushwa ya fedha imekuwa sababu kubwa ya kuzuia wanawake wengi kugombea nafasi za uongozi mbalimbali katika jamii,na kusababisha maendeleo ya mwanamke kurudi nyuma kwani lugha hiyo siyo njema katika usawa wa jinsia.

Hayo ya mesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Tamwa nchini Tanzania Rose Reuben ,na kusema kuwa lugha hizo dhalilishi ni lugha inayomfanya mwanamke ashindwe kuendelea mbele, kwa kuingiwa na woga ,kukosa ujasiri ,huku akihofia kudhalilishwa hadharani na kugombanishwa na jamii yake

Bi Rose amesema kazi kubwa ya Tamwa ni kuwajengea wanawake uwezo, kuhamasisha mazingira wezeshi ya wanawake kuwa viongozi, katika jamii ,siasa na katika uchumi haswa kipindi hichi kuelekea uchaguzi 28 octoba 2020 ambapo amesema ni kipindi cha kuzungumza na kuikumbusha jamii,kwamba mwanamke nae awe sehemu ya uongozi katika eneo la siasa

''Siyo suala kwamba tunapiga kampeni hapana tunaweka mazingira wezeshi kwa wananwake,tunawajengea wanawake uwezo pamoja na kuihamasisha jamii yetu, imeonekana kwenye jamii na yenyewe kuna kikwazo cha wanawake kuwa viongozi''alisema Rose.

Katika kuhamasisha suala la AMANI ,alisema kuwa mwanamke hawezi kugombania uongozi sehemu ambayo hakuna amani,fujo,vurugu,amesema tayari serikali ilishatangaza kuwa uchaguzi wa mwaka wa mwaka huu utakuwa wa huru, haki na amani ,hivyo wanasisitiza mwanamke naye awe sehemu ya uhuru, haki na amani kwani mazingira hayo yakiwepo watajitokeza wengi kuwania nafasi za uongozi

Ameitaka jamii kutambua kuwa ni kosa kutoa au kuomba rushwa ya ngono,amesema ni vyema kutoa taarifa pale jambo hilo linapojitokeza , amesema ni vyema kuweka kukumbuka au vizibiti kama ni ujumbe au ni simu iliyopigwa ili unapotakiwa kuvitoa katika sehemu husika uwe navyo kama moja ya ushahidi wao

Rose amesema kuwa jamii inapaswa kufahamu kuwa rushwa ya ngono haikubaliki na ni kosa kisheria,japo kuwa imekuwa haisemwi hadharani kwa muhusika kuhofia kudhalilishwa kwa kuogopa k ugombanishwa na wenzi wao na jamii kwa ujumla

Amesema katika mradi wa (wanawake sasa) unashughulika na vyama vitano vya siasa ambavyo ni CCM,CHADEMA,ACT,CUF pamoja na NCCR Mageuzi ambapo tayari baadhi yao wameshajengewa uwezo, pamoja na kutoa hoja mbalimbali zilizotoka katika midahalo waliyokuwa wakiiendesha.

''Sisi tunajiamini atii kwamba wanawake wanaweza yaani bidhaa tuliyonayo ambayo ni mwanamke inauzika wala hatuna wasiwasi ila tunachotaka mazingira yawekwe safitumefurahishwa sana idadi kubwa ya wanawake walijitokeza kuwania nafazi za uongozi katika ngazi ya udiwani,ubunge na hata Urais ''alisema Rose.

 

No comments :

Post a Comment