Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani), mara baada ya kukagua ubovu wa barabara ya
Nangurukuru hadi Mbwemkuru (km 155), iliyopo katika Barabara Kuu ya Dar
es Salaam hadi Lindi (km 452).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoka kukagua mzani wa
Nangurukuru uliopo mkoani Lindi wakati alipowasili mkoani humo kwa ajili
ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kukagua barabara ya kutokea Lindi
hadi Dar es Salaam na kutoridhishwa na hali ya miundombinu ya barabara
hiyo.
Naibu waziri wa Ujenzi, Elias
Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga, kuhusu
ukarabati wa sehemu iliyoharibiwa na malori ya mizigo ya mawe katika
barabara ya Mtwara – Lindi – Dar es Salaam.
Viongozi na Wataalam kutoka wizara
ya Ujenzi,uchukuzi na mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakisikiliza
maelezo kutoka kwa wasafirishaji wa mawe katika eneo la Kilanjelanje
mkoani Lindi tayari kwaajili ya kusafirishwa kuelekea jijini Dar es
Salaam.
Muonekano wa sehemu ya barabara
iliyoharibika kutokana usafirishaji wa mizigo kwa wingi baada ya
ongezeko kubwa la magari ya mizigo yanayotumia barabara hiyo ya Lindi –
Dar es Salaam na kupelekea kuharibu miundombinu ya barabara hiyo.
Lori la mizigo likipakia mawe
katika eneo la Kilanjelanje mkoani Lindi tayari kwaajili ya kusafirishwa
kuelekea jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ametengua nafasi ya
Meneja wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Pwani na Lindi kutokana na
kutoridhishwa na usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi ya barabara ya
Dar es Salaam – Kilwa – Lindi hadi Mingoyo yenye urefu takriban kilometa
450.
Aidha, ameagiza Mameneja wapya
wa mikoa hiyo na mameneja wa mikoa mingine kuhakikisha wanaziba mashimo
yote yaliyopo kwenye barabara zao ndani ya saa 48 kuanzia muda wa shimo
hilo linapojitokeza.
Mhandisi Kamwelwe, ametoa
agizo hilo akiwa mkoani Lindi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya
kutoridhishwa na hali ya miundombinu ya barabara kuanzia Nangurukuru
hadi Mbwemkuru wakati alipoikagua barabara hiyo siku chache zilizopita
ambapo pamoja na mambo mengine amesema kuwa hadi sasa bilioni 10
zimeshatengwa kwa ajili ya zoezi la kuziba mashimo yote kabla hayajaleta
athari zingine.
“Nimetengua nafasi za
watendaji hawa wawili kwa makosa yaliyojitokeza katika barabara hizi
zinazounganisha mkoa kwa mkoa na hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu
nahitaji wananchi wawe wanapita salama katika barabara hii”, amesema
Waziri Kamwelwe.
Waziri huyo ameeleza kuwa
sehemu kubwa ya barabara iliyoathirika ni kuanzia eneo la Muhoro mkoani
Pwani hadi Mbwemkuru mkoani Lindi yenye jumla ya urefu wa kilometa 190
na zote zipo katika utaratibu wa kuanza kukarabatiwa.
Waziri Kamwelwe amebainisha
kuwa ataendelea kusimamia muongozo wake alioutoa mwezi Juni mwaka huu
kuwa barabara yoyote yenye mashimo katika barabara kuu na za mikoa basi
huyo Mhandisi wa Mkoa ajiondoe mapema kwani hayuko tayari kufanya kazi
na wataalamu wasio weledi na kushindwa kusimamia rasilimali fedha na
watu vizuri.
Ameongeza kuwa hadi sasa
Serikali imeshatoa kiasi cha fedha bilioni 40 kwa ajili ya matengenezo
ya barabara zote nchini zilizoathriwa na maji ya mvua.
“Fedha zipo sasa sitarajii
kuona barabara yoyote hapa nchini ina mashimo, huyo Meneja ambaye
barabara zake zina mashimo tutamalizana hapo hapo”, amesisitiza Mhandisi
Kamwelwe.
Waziri Kamwelwe ameelezea
umuhimu wa barabara hiyo kiuchumi ambayo ilijengwa toka mwaka 2008 na
kusema kuwa ongezeko la usafiri wa abiria na usafirishaji wa bidhaa,
mazao na malighafi za viwandani katika kipindi cha miaka hii 12 ndiyo
imetuonesha namna ya kujipanga upya katika ukarabati wa barabara hii.
“Tunaleta watalaamu katika
barabara hii kwa ajili ya kuanza kusanifu upya na kuona kwanini
imeharibika kabla ya wakati wake na maandalizi yanaendelea vizuri”,
amefafanua Waziri Kamwelwe.
Katika hatua nyingine, Naibu
Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akiongozana na Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Arch. Elius Mwakalinga, wameikagua pia sehemu ya barabara hiyo na
kueleza kuwa hatua za awali za ukarabati zimeanza ambapo kazi hiyo
inatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, mwaka huu.
Naibu Waziri Kwandikwa
amewataka wakandarasi watakaopewa kazi ya ukarabati wa barabara hiyo
kukamilisha kabla ya kuanza kwa mvua za vuli zinazotarajiwa kunyesha
hivi karibuni kwani barabara hiyo ina mchango mkubwa sana wa kiuchumi na
kijamii kwa wakazi wa Nyanda za Kusini.
Naye, Katibu Mkuu Arch. Elius
Mwakalinga, amewahakikisha wakazi wa mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara
kuwa maeneo ya barabara yaliyokuwa yameharibika yameanza kufanyiwa
matengenezo kwa sababu asilimia 80 ya bajeti ya wizara imetengwa kwa
ajili ya ukarabati wa barabara nchini.
“Sina mashaka na kazi ya
ukarabati wa sehemu ya barabara hii kwa sababu fedha zipo na mimi nipo
eneo la tukio tangu Rais Magufuli alipotoa agizo la ukarabati wa
barabara hiyo na hadi sasa maandalizi yanaendelea vizuri”, alisisitiza
Arch. Mwakalinga.
Barabara ya Dar es Salaam hadi
Lindi inakarabatiwa kwa fedha za ndani na inatarajiwa kukamilika mwezi
Oktoba mwaka huu hii ikiwa ni hatua zili
No comments :
Post a Comment