Wednesday, August 19, 2020

KAIRUKI ATEMBELEA KIWANDA CHA KONYAGI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji  Mhe.Angellah Kairuki (kuia) akiongea na wafanyakazi wa Konyagi (TDL)  wakati  alipofanya ziara ya kikazi katika kiwanda hicho Chang”ombe  jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa kanda  ya Dar wa TDL, Deogratius Davis,  akitoa maelezo ya uendeshaji wa kampuni kwa Waziri Kairuki
Meneja wa Kiwanda cha Konyagi  (TDL ) Aranyaeli Ayo (Kushoto) akitoa maelezo ya uzalishaji bidhaa kwa Waziri Kairuki.
Waziri Kairuki na ujumbe wake wakitembezwa katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji wa bidhaa za TDL 

……………………………………………..

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki, akiongoza ujumbe wa maafisa kutoka wizara yake amefanya ziara ya kikazi katika kampuni ya Tanzania Distillers Limited (TDL) chini ya kampuni  ya TBL Group katika eneo la Chang’ombe jijini Dar es Salaam  na kujionea uzalishaji wa bidhaa zake na kusikiliza changamoto za uzalishaji  na mafanikio ya kampuni na mchango wake katika kukuza uchumi wa taifa sambamba na mkakati wake wa kufanikisha ajenda ya serikali ya Tanzania ya viwanda.

 

No comments :

Post a Comment