Kutoka
Kushoto ni Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bw. Ezra
Manjerenga,Kamanda Mkuu Mstaafu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga Bw.
John Shimba Kadama,Afisa Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara na Afisa
Mifugo Manispaa ya Shinyanga Bw. Chrispacy Kasimbazi wakiwa kwenye
studio za Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga.
Na Mwandishi wetu - Malunde1 blog
Wito umetolewa kwa Jamii kufuatilia vyombo vya Habari ili kupata
Elimu inayotolewa na wataalamu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Wanyama pori na wanyama wa Nyumbani kama vile mbwa na Paka.
Wito huo umetolewa leo na Maafisa wa Idara za Maliasili na Mazingira,Idara
ya Mifugo,Pamoja na Afisa kutoka Idara ya Utafiti na Afya,ambao kila mmoja ametoa
elimu kupitia kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Redio Faraja fm Stereo
kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa chini ya Mtangazaji Josephine Charles, juu ya
mahusiano yaliyopo kati ya Wanyama pori,wanyama wa nyumbani na Binadamu pamoja
na kutoa Elimu kuhusu Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa.
Akizungumza kupitia kipindi hicho Afisa Maliasili na Mazingira
wa Manispaa ya Shinyanga bwana EZRA MANJERENGA ametoa wito kwa Jamii kuondokana
na dhana potofu kwamba kuna fisi wanaofugwa
majumbani na badala yake wanapobaini kuwepo kwa mnyama huyo watoe taarifa kwa mamlaka
husika.
Kwa upande wake Afisa mifugo wa Manispaa ya Shinyanga Bwana CHRISPACY
KASIMBAZI ametumia nafasi hiyo kuwa hamasisha wakazi
wa Mji wa Shinyanga kupeleka mifugo yao kupata chanjo ili kuwa kinga na kifafa
cha mbwa,chanjo ambayo itaanza kutolewa kuanzia September Mosi hadi September 28 mwaka huu katika Manispaa ya Shinyanga.
Naye
afisa mtafiti kutoka taasisi ya Afya Ifakara Bwana JOEL
CHANGALUCHA ameiomba jamii kutoa taarifa kwa Mamlaka au taasisi husika
kupitia namba 0800750052 ambayo ukipiga ni bure ikiwemo idara
ya mifugo pale Mbwa ama Paka wao wanapoonekana kuwa na dalili za kichaa
cha
mbwa ili hatua stahiki ziweze chukuliwa.
Tazama picha chini.
Kutoka
Kushoto ni Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bw. Ezra
Manjerenga,Kamanda Mkuu Mstaafu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga Bw.
John Shimba Kadama,Afisa Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara na Afisa
Mifugo Manispaa ya Shinyanga Bw. Chrispacy Kasimbazi wakiwa kwenye
studio za Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga katika kipindi cha Mambo
leo Kinachoongozwa na Mtangazaji Josephine Charles.
Afisa
Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga akiwa
kwenye mahojiano maalum katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na
Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga.
Afisa Mifugo Manispaa ya Shinyanga Bw. Chrispacy Kasimbazi akiwa kwenye mahojiano maalum katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga.
Afisa Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara akiwa kwenye mahojiano maalum katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga.Kamanda Mkuu Mstaafu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga Bw. John Shimba Kadama akiwa kwenye mahojiano maalum katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga.
Kutoka
Kushoto ni Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bw. Ezra
Manjerenga,Kamanda Mkuu Mstaafu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga Bw.
John Shimba Kadama,Mtangazaji wa Kipindi cha Mambo leo Radio Faraja fm
stereo Josephine Charles,Afisa Mifugo Manispaa ya Shinyanga Bw. Chrispacy Kasimbazi na Afisa Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara wakiwa katika picha ya Pamoja nje ya Studio za Radio Faraja baada ya Kipindi.
No comments :
Post a Comment