Meneja
wa Benki ya CRDB, Kanda ya Kaskazini Chiku Issa (Kushoto) akiwa na
Mchimbaji madini Bilionea, Saninio Laizer (wa pili Kushoto), Meneja wa
Biashara wa Kanda (CRDB), David Peter (Mwenye Miwani) na Meneja wa tawi
la Mirerani kwa benki hiyo, David Ndohele. (Picha na Pamela Mollel).
Meneja
wa Benki ya CRDB Chiku Issa akizungumza na vyombo vya habari katika
eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite Mirerani (Picha na Pamela
Mollel).Meneja wa Benki ya CRDB, Kanda ya Kaskazini Chiku Issa (wa tatu kulia) akimpongeza Mchimbaji madini Bilionea, Saninio Laizer (Kushoto).
Picha ya pamoja
Na Pamela Mollel, Mirerani
Benki
ya CRDB imeanza mkakati wa kujenga tawi lake jingine na la kwanza
katika eneo la uchimbaji madini la Mirerani, hususani ndani ya ukuta
mkuu wa Magufuli.
Meneja
wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Chiku Issa amesema taaasisi hiyo
ya fedha ina madhumuni ya kupeleka huduma za kibenki karibu kabisa na
wachimbaji wote wadogo kwa wakubwa wa eneo la Mirerani, maarufu kwa
machimbo ya madini ya vito aina ya Tanzanite.
“Pia
kuhakikisha kuwa miamala ya ununuzi na uuzaji inafanyika ki usahihi na
kwa wakati, na vile vile kuwezesha ulipwaji wa kodi za serikali,”
alisema Chiku ambaye aliongeza kuwa yeye binafsi amefika Mirerani
kujifunza namna ya uchimbaji na uuzaji wa madini unavyoendeshwa ili
aweze kuwasaidia wahusika.
Kwa
mujibu wa meneja huyo, benki yake pia itawasaidia wachimbaji katika
kuwapatia mikopo mbalimbali kuwasaidia katika mitaji na ununuzi wa vifaa
vya shughuli zao kama mashine za kuchimbia na kuhudumia migodi yao.
Chiku
ameeleza pia wanatoa pia ushauri kwa wachimbaji, akiwemo bilionea mpya
Saninio Laizer, wa jinsi ya kuwekeza pesa zake kwa ajili ya kupata faida
Zaidi. “Yeye ni mteja wetu mkubwa!” alisema.
No comments :
Post a Comment