Tuesday, July 14, 2020

WHO: Janga la Corona litaendelea kuwa baya zaidi

Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
JANGA la Corona litaendelea kuwa ‘Baya na baya zaidi’ ikiwa Serikali zitashindwa kuchukua hatua
madhubuti, Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha.
Mkuu wa shirika hilo Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “Nchi nyingi sana zimekuwa zikielekea kwenye njia ambayo sio isiyo sahihi,”
“Idadi ya watu walioambukizwa ilimekuwa ikiongezeka kwenye maeneo ambayo masharti yalikuwa hayafuatwi”.
Marekani imeshuhudia ongezeko la maambukizi wakati kukiwa na mvutano kati ya wataalamu wa afya na Rais Donald Trump.
Nchi iliyoathirika zaidi dunian ikiwa na zaidi ya watu milioni 3.3 walioathirika na vifo zaidi ya 135,000 kwa mujibu wa Chuo cha Johns Hopkins.
Dkt.Mike Ryan ni Mkurugenzi wa dharura kutoka WHO amesema tunapaswa kujifunza kuishi na virusi, na kutahadharisha kutokuwepo kwa matarajio kuondoshwa kwa virusi na chanjo kuwa tayari kwa miezi kadhaa.
Amesema kuwa bado haijajulikana kupona kwa ugonjwa wa Covid-19 kutasababisha kuwa na kinga, na ni kwa muda gani kinga hiyo itakuwepo mwilini.
Utafiti huo umetolewa mapema wiki hii na wanasayansi kotoka Chuo cha Kings Jijini London umesema kuwa kinga dhidi ya virusi inaweza isiwe ya muda mrefu.

No comments :

Post a Comment