Waziri
wa Viwanda na Biashara, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina
Sa;lum Ali (kushoto), akimkabidhi tuzo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF), Masha Mshomba, baada ya kuibuka mshindi wa
muoneshaji bora kundi la Taasisi za bima na hifadhi ya jamii, katika
maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yaliyofikia
kilele leo Julai 13, 2020 katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es
Salaam.
Mshomba akionyesha tuzo hiyo mbele ya banda la WCF viwanja vya Julius Nyerere, maarufu Sabasaba mara baada ya kukabidhiwa.
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetwaa tuzo ya mshindi wa
kwanza ya muoneshaji bora kundi la Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi
ya Jamii kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba amepokea tuzo hiyo kutoka kwa
Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi
Amina Salum Ali wakati wa kilele cha maonesho hayo yaliyofanyika kwenye
viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam leo
Julai 13, 2020.
“Kusema kweli siku ya leo tunayo furaha sana mimi mwenyewe na
wafanyakazi wenzangu wote, kwa mara ya kwanza tumeweza kushika nafasi ya
kwanza katika sekta ya bima na mifuko ya hifadhi ya jamii, hii
inadhihirisha kwamba penye nia pana njia, mwaka jana tulikuwa washindi
wapili tukaweka azma kwamba walau siku moja tuwe washindi wakwanza na
leo imefika tunashukuru sana.” Amesema Mshomba na kuongeza…
Ushindi huu unaendana na vision ya Mfuko, tumejiwekea malengo ya kuwa
taasisi ya kuigwa sio tu hapa Tanzania lakini Afrika hususan katika
taasisi za hifadhi ya jamii na haswa katika Mifuko ya Fiadia na
tunapokuwa wakwanza katika maonesho haya makubwa hapa nchini hiyo
inaonyesha kwamba tumko katika njia sahihi na lengo letu ni kuendelea
kushika nafasi kama hizi katika maonesho na shughuli mbalimbali
tunazoshiriki.
“Huduma zetu ni bora tumeboresha sana huduma zetu na kwa sasa
zinapatikana kupitia mtandao (online portal) na waliofika katika banda
hili wameelezea jinsi walivyovutiwa na huduma zetu zote zinapatikana
kupitia mtandao na ule usumbufu kwa wateja haupo kabisa kwa sababu Mafao
yanalipwa kupitia mtandao, lakini hata taarifa za kutokea ajali au
kuumia kazini zinawasilishwa kupitia mtandao, usajili wa waajiri na
wanachama wenyewe ni kupitia mtandaoni, , kitu kwa sasa tunafanya
kupitia mtandao, usajili wa waajiri ni kupitia mtandao, ukusanyaji wa
michango ni kupitia mtandaoni kwahivyo kila kitu tunafanya kwa kutumia
mtandao na hilo kwakweli limewezesha kuboreshwa kwa shughuli zetu na nia
yetu kwakweli ni kuwa kileleni.” Amefafanua Mshomba.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Masha Mshomba akiungana
na wafanyakazi wa Mfuko waliokuwa wakihudumia wananachi waliotembeela
banda hilo wakati wakisherehekea ushindi huo.
No comments :
Post a Comment