Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kuzindua ununuzi wa pamba Mkoani Katavi kwa msimu wa 2020/2021 kwenye Chama cha Msingi cha Ushirika cha Kasekese wilayani Tanganyika, Julai 4, 2020.
====== =============== ================
*Awataka
wasiwe madalali wa kuingiza wahamiaji haramu nchini
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka watu wanaoishi kwenye makazi ya
Mishamo na Katumba wawe waadilifu na wasitumike kama madalali wa kuingiza
wahamiaji haramu nchini.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mkoa wa Katavi umekithiri kwa kuwa na
wahamiaji haramu wengi, hivyo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera
ashughulikie tatizo hilo.
Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Julai 4, 2020) alipozindua jengo la
ofisi na biashara la Mpanda Plaza lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
mjini Mpanda kwa gharama ya sh bilioni
2.8.
“Katavi imetulia lakini
haijatengamaa kwa sababu ni kati ya mikoa yenye idadi kubwa ya wahamiaji haramu
nchini ambao njia yao wanayotumia kuingilia Katavi ni makazi ya Katumba na Mishamo.”
Waziri Mkuu amesema Tanzania
haijazuia watu wa Mataifa mengine kuingia nchini ila inawataka wafuate taratibu
zilizowekwa na si kuingia kwa kutumia njia za panya.
Amesema anamajina ya watu zaidi
2,000 walioingia Tanzania kwa njia za panya na wamejiingiza katika maeneo
mbalimbali, amewataka warudi kwao na
wafuate taratibu kabla ya kuja tena nchini.
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa
Mpanda Plaza, Waziri Mkuu ameliponeza Shirila la Nyumba la Taifa kwa uwekezaji
huo ambao utaliwezesha shirika hilo kujiongezea tija.
Kadhalika, Waziri Mkuu
amelielekeza shirika hilo kwenda kujenga majengo ya makazi katika wilaya mpya
ili kuwawezesha watumishi na wananchi kuishi kwenye makazi bora.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dkt. Maulidi Banyani amesema uzinduzi
wa jengo hilo la ghorofa tano ni muendelezo wa miradi iliyowekezwa na NHC kwa
gharama ya sh bilioni 7.2 mkoani Katavi.
Dkt. Banyani amesema miradi
mingine iliyowekezwa na NHC mkoani Katani ni pamoja na ujenzi wa nyumba 70 eneo
la Ilembo, nyumba 24 katika mji wa Inyonga, Mlele.
“Tumejenga nyumba tano za Wakuu
wa Idara halmashauri ya Wilaya ya Mlele, nyumba 24 za walimu katika shule ya
msingi Kakuni, nyumba sita shule ya Kibaoni halmashauri ya Mpimbwe.”
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, alisema miongoni mwa changamoto
zilizokuwa zinaukabili mkoa huo ni majangili ambapo waliendesha operesheni na
kufanikiwa kikamata silaha 100.
Alisema kwa sasa wananchi
wanaendelea kufanya kazi na kwamba ukusanyaji wa mapato umeongeza kutoka
asilimia 76 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 97 mwaka huu.
Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa
mbali na kuboresha ukusanyaji wa mapato, pia wameimarisha upatikanaji huduma za
afya hususani kwa mama na mtoto.
No comments :
Post a Comment