Thursday, July 2, 2020

WAMILIKI WA VIWANDA VYA KUSAMBAZA VIFAA VYA UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME WATAKIWA KUZALISHA VIFAA VYENYE BORA

   
……………………………………………………………………….
Na.Farida Saidy, Morogoro
Serikali imeagiza viwanda vyote vilivyopewa tenda ya kusambaza vifaa vya ujenzi katika
mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere mw 2115 kuhakikisha wanazalisha vifaa vitakavyokidhi ubora wa kazi hiyo inayogharimu fedha nyingi za serikali ili kodi za watanzania kutumikakiharari.
Kauli hiyo Naibu waziri wa viwanda na biashara Mhandisi Stella Manyanya wakati alipotembelea mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere mw 2115.
Aidha Manyanya amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa nchini ambao ujenzi wake ukiwa umehusisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na sekta binafsi hivyo amewataka wenyeviwanda kupeleka malighafi zenyeubora.
Manyanya ameupongeza Uongozi wa shirika la umeme tanzania TANESCO kwa kuwa wasimamizi zuri wa maradi huo ambao utawasaidia watanzania kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuri mbalimbali ikiwemo kufungua viwanda vitakavyozarisha ajila kwa vijana.
Katika Kuwasilisha taarifa ya hali yautekelezwaji wa mradi huo mhandisi mkazi Mushubila Kahumbwa amesema mradi utakapokamilika utajumuisha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya uvuvi,kilimo,viwanda pamoja na utalii,hali itakayopelekea kukuza uchumi wa watanzania na taifa kwa ujumla.
Naye Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu amewataka watanzania waliobahati kapata ajila katika mradi huo kufanya kazi kwa juhudi kubwa ili kufanikisha adhima ya serikali ya kukamisha mradi huo ifikapo juni 2022.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania Muhandisi Khalid James amesema wao kama wasimamizi wakuu wa mradi huo watahakikisha wanamsimamia vizuri mkandarasi katika kila hatua atakayofikia ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na uboara uliokusudiwa.

No comments :

Post a Comment