Afisa
Lishe Mtafiti Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na
lishe Tanzania, Bw. Walbert Mgeni akitoa ufafanuzi wakati akifanya
mahojiano na mwandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu
mama kunyonyesha mtoto.
******************************
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Wazazi wametakiwa kutambua umuhimu
kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama katika
kipindi cha miezi sita
hadi miaka miwili ili kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima ikiwemo saratani
ya matiti.
Akizungumzia umuhimu wa wiki ya
unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama Duniani, Afisa Lishe Mtafiti Idara ya
Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na lishe Tanzania, Bw.
Walbert Mgeni, amesema kuwa kila mwaka kuanzia mwezi Agosti 1 hadi 7
Tanzania inaungana na nchi nyengine duniani kuadhimisha wiki ya
unyonyeshaji.
Bw. Mgeni amesema kuwa wazazi
wanatakiwa kutambua maziwa ya mama ni muhimu hususani kwa watoto katika
kipindi cha miezi sita, kwani maziwa hayo yanavirutubisho ambavyo
vinazuia magonjwa mbalimbali kwa mtoto.
Amesema kuwa watoto wachanga
wanapaswa kuanza kunyonyeshwa maziwa ya mama ndani ya saa moja baada ya
kuzaliwa ili maziwa yaanze kutoka mapema.
“Kumnyonyesha mtoto ndani ya saa
moja baada ya kuzaliwa kuna faida nyingi ikiwemo kusaidia maziwa ya mama
kuanza kutoka mapema na mtoto kupata maziwa ya mwanzo ya njano” amesema
Bw. Mgeni.
Mtaalam huyo ameeleza kuwa kuna
maziwa ya njano ambayo ni maziwa ya mwanzo, mazito yenye rangi ya njano
utoka siku chache za mwanzo baada ya kujifungua.
Amesema kuwa maziwa hayo ni chakula kamili chenye virutubisho vingi, na pia yanatoa kinga maalum dhidi ya maradhi.
Licha mtoto kupata virutubisho
akitumia maziwa ya mama, lakini kuna faida nyingi kwa mama kunyonyesha
ikiwemo msaidia kuepuka kupata magonjwa ya saratani ya matiti.
Amefafanua kuwa kuna changamoto
zinazokabili khali ya lishe kuwa ni kuamini mila na destuli potofu
watoto kuachishwa kunyonyeshwa mapema pamoja na uelewa mdogo kuhusu
maswala unyonyeshaji.
Katika kukabiliana na changamoto
hizo wanaendelea kutoa elimu ya unyonyeshaji na lishe ili kuhakikisha
watanzania wanakuwa na afya bora
No comments :
Post a Comment