Na Zainab Nyamka, Michuzi TV.
UJENZI
wa Mradi wa Maji wa Mkuranga umefikia asilimia asilimia 80 unaendelea
kutekelezwa kwa kasi ili kukamilika kwa wakati na wananchi kuanza kupata
huduma ya maji safi.
Mradi
huo unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam DAWASA unahusisha ujenzi wa tanki la lita milioni 1.5 na ulazaji
wa mabomba ya usambazaji.
Ujenzi
wa mradi huo ni muendelezo wa kisima walichochimba eneo la kurungu
mwaka 2015 ukijengwa kwa thamani ya bilioni 5.5 kupitia mapato ya ndani
utajumuisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita milioni 1.5 tenki la
kupokea na kusambaza maji hadi kwenye tanki sambamba na ulazaji mambomba
urefu wa kilomita (63) hadi Vikindu.
Maeneo yatakayonufaika kuwa ni pamoja na Mkuranga A,B,Kiguza,Bigwa,sambamba na Mkwalia Kitumbo,Njia Nne, Hoyoyo.
Mradi
huo utakapomalizika utahudumia wakazi 25,500 sawa nan asilimia 83
ambapo kwa sasa jumla ya wakazi 4500 sawa na asilimia 17.6 ndiyo
wanaopata maji safi na salama.
No comments :
Post a Comment