Kifaa cha Kudetect Madini kwenye Miamba Bidhaa ya Madini yaliyotoa vitu vya thamani
NA EMMANUEL MBATILO
Tume ya Madini imeweza kuvuka
lengo walilopewa la ukusanyaji wa mapato kwani mwaka 2019-2020 walipewa
lengo la kukusanya Bilioni 470 hivyo wao wamevuka na kukusanya Bilioni
528.2.
Akizungumza katika banda la tume
hiyo katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar Es
Salaam, Mtakwimu wa Tume ya Madini Bw.Azihar Kashakara amesema kuwa
tume
imekuwa na mchango mkubwa katika pato la Serikali hadi kufikia nchi
kwenye uchumi wa kati.
“Kupitia Tume ya Madini kuweza
kukusanya kwa makini tozo mbalimbali zinazotokana na shughuli mbalimbali
za madini zimeweza kusaidia kuwa na mchango mkubwa nchi kufikia uchumi
wa kati”.Amesema Bw.Kashakara.
Kwa upande wake Meneja Habari na
Mawasiliano-Tume ya Madini Bw.Greyson Mwase amesema katika Maonesho ya
mwaka huu Tume ya Madini imeweza kushirikisha wachimbaji wadogo na
waongezaji thamani madini na wametumika kama mfano wa kuwahamasisha
wananchi ambao wanania ya kuingia kwenye uchimbaji mdogo wa madini.
“Maonesho yamekuwa na manufaa na
tumejiandaa kikamilifu na tutaendelea kushiriki forum mbalimbali
kwaajili ya kuhakikisha wawekezaji kutoka nje ya nchi wanakuja kuwekeza
hapa nchini katika sekta ya Madini na hasa ukizingatia nchi yetu
tumeingia kwenye nchi yenye kipata cha kati na sisi tutaendelea kufana
vizuri zaidi huku tukihakikisha sekta ya madini inakuwa na mchango
mkubwa”. Amesema Bw.Mwase.
Aidha Bw.Mwase amesema wananchi
wengi wamekuwa wakija kuulizia kuhusiana na namna gani wanaweza
kujiingiza kwenye shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na taratibu za
kupata leseni.
Hata hivyo Bw.Mwase amesema wengi
wamesikia masoko ya madini yaliyoanzishwa hivyo basi wengi wameonesha
nia ya kufanya biashara ya madini kutumia mfumo wa masoko ulioanzishwa.
“Wananchi wameweza kuelimika hivyo
kupitia soko la madini litaenelea kukua zaidi kutokana wengi kuwa na
uelewa mkubwa namna ya kuendesha biashara ya Madini”.Amesema Bw.Mwase.
No comments :
Post a Comment