Wednesday, July 1, 2020

TEKNOLOJIA KURAHISISHA USAHILI YAJA TANZANIA

July 1, 2020, Dar es Salaam, Tanzania
Kampuni ya usahili Tanzania imeunda na kuzindua mfumo wa kupima uwezo na ufanisi wa waajiriwa kupitia teknolojia.
 Zana hiyo iliyopewa jina la ‘Skills Assessment Tool’ au ‘Zana ya Tathmini ya Ujuzi’ imeundwa kwa lengo la kuwapunguzia waajiri changamoto wanazokumbana nazo katika mchakato wa usahili hasa katika kupitia mamia ya CV wakati wa mchakato wa kuajiri. 
Teknolojia ya Skills Assessment Tool inawezesha waajiri kuchuja maombi ya nafasi ya kazi na kuwawezesha kupata waombaji wachache pekee waliokidhi vigezo vya kazi husika. 
Waombaji watafanyiwa tahmini ya awali katika mchakato wa usahili kupitia Zana ya Tathmini ya Ujuzi, teknolojia ya tahmini ambayo hupima uwezo wa waombaji zaidi ya ilivyo kwenye wasifu (CV) zao. 
Zana hii huchuja uwezo wa msingi na stadi ngumu zinazohitajika kwa jukumu fulani lililotangazwa.
 Matokeo ya tahmini huwasilishwa kwa mwajiri kupitia mfumo wa kufuatilia waombaji (ATS), dashibodi ya mwajiri ambayo inayomwezesha kuchuja waajiri bora zaidi kulingana na vigezo tofauti, pamoja na alama za majaribio.
Akifafanua kuhusu teknolojia hii, Mkurugenzi Mtendaji wa BrighterMonday Tanzania Reshma Bharmal-Shariff amebainisha namna ambavyo waajiri wanavyojikuta katika wakati mgumu hasa pale wanapozungukwa na idadi kubwa ya waombaji wa kazi wasio na sifa stahiki. 
“Teknolojia imerahisisha upatikanaji wa taarifa na michakato ya kuomba ajira, hii imepelekea kwamba mtu yeyote anaweza kuomba kazi yoyote bila kujali vigezo mahsusi vya kazi husika. Hii inawasababishia maumivu Maafisa Rasilimali Watu kwani wanajikuta wana CV nyingi za kufanyia tathmini kabla ya kupata waombaji wachache watakaofaa kwa usahili. " Alielezea Reshma. 
"Hii ndio sababu tuliona haja ya kuwasaidia waajiri kutambua ni mwombaji gani mwenye ujuzi stahiki wa nafasi hiyo. Mwajiri sio lazima apitie mamia ya CV tena, kutafuta mwajiri fulani. Waombaji wenye sifa wapo, na teknolojia hii inampa uwezo mwajiri kumpata mwajiriwa sahihi kwa kubonyeza vitufe vichache katika kompyuta yake. Kupitia zana hii, mwajiri anaweza kutazama alama za mwombaji na vigezo vingine kama vile kiwango cha elimu na uzoefu. Kwa njia hii, mwajiri anaweza kulinganisha ustadi, sifa, na viwango vya uzoefu kwa muda mfupi",Reshma Bharmal-Shariff alihitimisha. 
Zana hii imeleta ufanisi mkubwa kwa waajiri nchini Tanzania kwani sasa wanaweza kuchagua waombaji wenye uwezo zaidi bila upendeleo, na kwa kutumia vigezo vinavyokidhi mahitaji ya mwajiri husika.

No comments :

Post a Comment