Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati.
…………………………………………………………………………..
Na John Walter-Babati
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara inamshikilia
mfanyabiashara Japhet Samwel Alute kwa kukwepa
kulipa kodi ya serikali na kufanya biashara bila kuwa na leseni.Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara inamshikilia
Mkuu wa Takukuru mkoani
hapa Holle Makungu amesema kuwa mtu huyo pia anatoa mikopo umiza kwa
wananchi kwa riba kubwa na kisha kuwadhulumu mali zao wanazoweka kama
dhamana.
Makungu amesema kuwa
Alute pia anawatishia wananchi wanaochelewa kufanya marejesho kwa
kutumia jina la Halmashauri ya Mji wa Babati kwa kuwatumia ujumbe wa
kuwauzia maeneo yao au nyumba walizoweka kama dhamana kwa mikopo umiza.
Amesema katika upekuzi
walioufanya kwa mfanyabiashara huyo wamekuta mikataba ya kitapeli 99
ambayo inaonyesha ameuziwa maeneo mbalimbali zikiwemo nyumba na viwanja
vya baadhi ya wananchi wa Mji wa Babati.
Aidha mtuhumiwa amekutwa akiwa na vitambulisho vya watumishi wa Umma na uraia wa Tanzania ambavyo si Mali yake.
Mkuu huyo wa TAKUKURU
Mkoa wa Manyara Holle Makungu ametoa wito kwa wote waliokumbana na
mikopo hiyo umiza ya Alute au Mali zao kuchukuliwa kutokana na mikopo
hiyo, wafike Ofisi za Takukuru Manyara Mtaa wa Miomboni mjini Babati
siku ya Jumatatu Agosti 3,2020 ili Changamoto za mikopo umiza ziweze
kupatiwa ufumbuzi.
No comments :
Post a Comment