Sehemu
ya ujumbe ulioambatana na Mhe. Prof. Kabudi ukifuatilia mazungumzo kati
ya Prof. Kabudi na Balozi Huang Xia (hawapo pichani). Kulia ni Bw.
Magabilo Murobi, Katibu wa Waziri na Bw. Ali Ubwa, Afisa Mambo ya Nje.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Prof.
Kabudi ateta na Mjumbe Maalum wa Maziwa Makuu
Dodoma, 2 Julai 2020Tanzania
inaamini katika umoja wa jumuiya ya kimataifa kwenye
kutafuta ufumbuzi
wa changamoto zinazoikabili dunia ikiwemo mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) alipofanya
mazungumzo kwa njia ya mtandao na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa kwenye eneo la Maziwa Makuu, Balozi Huang Xia.
Viongozi
hao walitumia fursa hiyo kubadilishana mawazo katika masuala mbalimbali
yanayotokea duniani, ikiwa ni pamoja na mikakati na mbinu bora za
kukabiliana na janga la ugonjwa wa Corona na athari zake katika uchumi
kwenye eneo la Maziwa Makuu.
Balozi
Huang alielezea hatua mbalimbali anazozichukua zikiwemo kuongea na
taasisi za kimataifa za fedha na wadau wengine kwa ajili ya kuzihimiza
kutoa misaada kwa nchi za Maziwa Makuu ili ziweze kukabiliana na janga
la ugonjwa wa Corona na athari zake za kiuchumi na kijamii. Licha ya
kukutana na taasisi hizo, Balozi Huang pia amefanya mashauriano na
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Maziwa Makuu kuhusu janga la Corona.
Kwenye mashauriano hayo Mawaziri wamesisitiza umuhimu wa kuandaa mkutano
wa Mawaziri kwa njia ya mtandao ili kujadili, pamoja na mambo mengine
mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona na hali ya usalama katika
eneo la Maziwa Makuu.
Kwa
upande wake, Prof. Kabudi aliunga mkono wazo la kuwa na mkutano wa
Mawaziri wa nchi za Maziwa Makuu na kuelezea matumaini yake kuwa,
mkutano huo utatoa mawazo mazuri yatakayosaidia ufumbuzi katika
changamoto zinazoikabili dunia ukiwemo ugonjwa
wa Corona.
Aidha,
Prof. Kabudi alitoa maelezo kuhusu mikakati iliyochukuliwa na Serikali
ya Tanzania katika kudhibiti ugonjwa wa Corona. Alisema moja ya mikakati
hiyo ni tangazo la maombi ya siku tatu kwa nchi nzima lililotolewa na
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, maombi ambayo yaliyohusisha imani
zote. Tangazo hilo lilionekana ni jambo geni kwa watu wengi duniani
lakini kwa Tanzania, nchi yenye waislamu na wakristo takribani nusu kwa
nusu, lilikuwa ni muhimu na uamuzi huo haukuifanya Tanzania kupuuza
maelekezo mengine
yanayotolewa na wataalam wa afya.
Mazungumzo
hayo yalihitimishwa kwa Mhe. Waziri kuahidi kuwa, Tanzania
itashirikiana kwa karibu na ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
katika uamuzi wake wa kuandaa mkakati maalum wa kuzuia migogoro na
kuimarisha amani na utulivu kwenye eneo la nchi za maziwa makuu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
|
No comments :
Post a Comment