**************************
Na Magreth Mbinga
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh
Paul Makonda amewapatia kazi TAKUKURU ya kuchunguza 10% ya pesa
zinazotolewa na Serikali kwaajili ya kukwamua Wanawake,Vijana na
walemavu Kama zimewafikia walengwa na kutoa majibu kabla ya tarehe 20
mwezi wa 7 mwaka huu.
Hayo ameyazungumza leo wakati wa
kukabidhi miradi iliyopo katika Wilaya ya Ubungo alipokuwa akikagua
vikundi vya ujasiliamali vilivyopata mkopo kutoka Serikalini .
“Serikali imetoa Bilioni 33
kwaajili ya kukwamua wamama,walemavu na vijana sina uhakika
kama fedha
hizo zinawafikia walengwa TAKUKURU fanyeni uchinguzi na majibu
yapayikane kabla ya July 20 mwaka huu”amesema RC Makonda.
Pia amesema kuanzia leo July 1
Mkoa wa Dar es Salaam umerudi rasmi kwenye shughuli zake za kawaida watu
wafanye kazi na wamiliki wa hoteli,baa,kumbi na biashara mbalimbali
watembee kifua mbele kwasababu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
ni Mchamungu zipo nchi mpaka sasa wanajifungia ndani kwaajili ya janga
la Corona.
Vilevile Rc Makonda amekabidhi
miradi mingine kama upanuzi wa barabara kutoka Shukikango kwenda Bamaga
yenye urefu wa km 3.7 ,upanuzi wa hospitali ya Palestina ambayo itakuwa
ya ghorofa 4 itakayoweza kuhudumia wagonjwa 2000 baada ya kukamilika .
Sanjari na hayo pia amekabidhi
mradi wa mto ng’ombe ambao Ni miongoni mwa mito 8 mikubwa ya Jijini Dar
es Salaam ambao utamwaga maji mto msimbazi na utaghalimu Bilioni 32
kukamilika.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Urafiki
Motorcycle Group Husein Kamote ameishukuru Serikali kwa kuwapatia mkopo
usio na riba ambao umewakwamua kimaisha .
No comments :
Post a Comment