Monday, July 6, 2020

Rais Magufuli awasimamisha kazi viongozi wa polisi, Afisa Usalama kwa uzembe

Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru na Afisa Usalama wa Wilaya hiyo mkoani Arusha kwa kushindwa kutumiza majukumu yao.

Akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Rais Magufuli amesema kuwa viongozi hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kukabiliana na dawa za kulevya, hadi maofisa kutoka makao makuu walipofika na kubaini uwepo wa kiwango kikubwa cha bangi.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amempandisha cheo James Kaji kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ambapo awali alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Akitangaza uamuzi huo wa kumthibitisha Kaji pamoja na kumuapisha, Rais Magufuli amesema anachotaka kuona ni matokeo ya kazi wanazofanya wasaidizi wake.

No comments :

Post a Comment