Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
NBC, Theobald Sabi (kushoto), akionyesha tuzo ya udhamini mkuu wa
maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, mara baada ya
kukabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Balozi Amina
Salum Ali, katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonesho hayo katika
Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam hivi karibuni. Wa pili kulia ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko wa Tanzania, Prof.
Riziki Shemdoe.
Waziri wa Viwanda na Biashara wa
Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), kwa kutambua mchango wa NBC
katikakudhamini Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba
yalimalizika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wa pili kulia ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko wa Tanzania Bara, Prof.
Riziki Shemdoe.
Mfanyabiashara bilionea wa
Tanzania wa madini ya Tanzanite, Saniniu Laizer (kulia), akipata maelezo
ya huduma za kibenki zinazotolewa na NBC alipotembelea katika banda la
benki hiyo wakati wa Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es
Salaam katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC,
Theobald Sabi (katikati) akipozi kwa picha ya kumbukumbu na baadhi ya
maofisa wa benki hiyo katika banda lao wakati wa Maonesho ya 44 ya
Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba
jijini Dar es Salaam hivi karibuni
………………………………………………………………………..
BENKI ya Taifa ya
Biashara (NBC), imewataka wajasiriamali kutumia huduma bora za
kibenki
za NBC ili kunufaika na bidhaa mahususi zinazowalenga wafanyabiashara
wadogo na wa kati ikiwemo mikopo isiyohitaji dhamana.
Hayo yalisemwa
jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC,
Elvis Ndunguru alipokuwa akizungumzia udhamini wao katika Maonesho ya
Kimataifa ya Biashara ya Dar e salaam (DITF), ambapo alisema benki hiyo
iliweka nguvu nyingi katika upande wa wafanyabiashara wadogo na wa kati
katika kuonesha huduma zao.
“Benki ya NBC
inajivunia mchango wake mkubwa inaoutoa katika kusapoti wafanyabiashara
wadogo na wa kati jambo lililoipaisha benki yetu mwaka jana kuwa moja
kati ya benki tano bora barani Afrika katika biashara ya sme’s ikiwa ni
moja ya mafanikio makubwa kwa NBC kwa mwaka 2019”, alisema.
Mkurugenzi
huyo aliongeza kuwa NBC ilishinda tuzo hiyo kutokana na sababu
mbalimbali moja ikiwa ni huduma zao wanazozitoa na mikopo ya aina
mbaimbali ikiwemo mikopo ambayo haihitaji dhamana kabisa na inayotoka
kwa muda mfupi kwa ajili ya wajasiliamali wadogowadogo.
“NBC katika
kuonyesha kuwa tunawathamini wafanyabiashara hawa na kutambua umuhimu wa
mchango wao katika kuchangia uchumi wa Taifa na pia kuboresha biashara
zao ndio maana kwa maonesho ya mwaka huu tumedhamini banda maalumu la
wajasiriamali hao tuliowatoa katika ngazi ya chini na sasa wakiwa katika
ngazi ya juu ili waoneshe biashara zao”, alisema Bwana Ndunguru.
Aidha mkurugenzi
huyo alisema NBC inatoa pia huduma Huduma ya kuwaongezea uwezo
wajasiriamali katika shughuli zao mfano ikiwa ni pamoja na kujifunza
utunzaji wa kumbukumbu, namna bora ya ulipaji wa kodi za Mamlaka ya
Mapato (TRA) na pia kupanua wigo wa biashara zao kwa safari za kimafunzo
nje ya nchi ikiwemo China na nchi nyingine.
No comments :
Post a Comment