Wednesday, July 1, 2020

NAIBU WAZIRI KANYASU APONGEZA HOTELI YA SERENA KUFUNGULIWA BAADA YA JANGA LA CORONA



Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu leo wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Hoteli ya Serena iliyopo Jijini Dar es Salaam  baada ya janga la Corona kufuatia kufungwa kwa takribani miezi mitatu ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya ugonjwa huo, Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa  Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto, Godwin Mollel na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo pamoja na Wadau wengine wa Utalii.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto  Mhe.Anthony Mavunde akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Constantine Kanyasu pamoja na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Dkt.Godwin Mollel pamoja na wadau wengine wa Utalii wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya kufungua Hoteli ya Serena iliyokuwa imefungwa kwa takribani miezi mitatu ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya ugonjwa wa Corona
.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona
 Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)  Jaji Mstaafu Thomas Mihayo  wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua matukio wakati wa ufunguzi rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona.
Naibu Waziri wa  Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto,  Dkt. Goldwin Mollel  akizungumza wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya CoronaNaibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akizungumza wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona.
*************************************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amepongeza uamuzi wa Hoteli ya Serena wa kufungua hoteli hiyo tangu ilipofungwa kwa ajili ya kuweza  kukabiliana na
mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona.
Amezitoa pongezi hizo  leo Jijini Dar es Salaam wakati akishiriki hafla ya kufungua hoteli ya Serena ambayo imekuwa ni muhimu katika kuwahudumia Watalii wengi wanaotoka na kuingia kutoka  Nchi za nje kabla na baada ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.
Amesema uamuzi huo wakufungua hoteli hiyo  unatoa ujumbe mzito Duniani     kuwa Tanzania ipo salama na ipo tayari kwa ajili ya kuwapokea Watalii.
Amesema kurudi kwa biashara hiyo kunarudisha uhakika wa maisha ya watu takribani 450,000 ambao wameajiriwa moja kwa moja katika sekta ya Utalii.
Amesema Ugonjwa wa Corona uliiathiri jamii katika nyanja za  kiuchumi na kijamii baada ya watu wengi kupoteza ajira zao na wengine kuachishwa kazi kutokana na janga hilo
Amesema uamuzi huo wa Hoteli ya Serena kuifungua hoteli hiyo kunaleta mwanga wa matumaini kwa Watanzania wanaoitegemea Sekta ya Utalii katika kuendesha maisha yao.
” Ninawashukuru Hoteli ya Serena kwa kupeleka ujumbe kwa Wawekezaji wetu wote ambao wanaogopa na kufunga biashara zao kwa ajili ya Ugonjwa huo.
Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Virusi vya  Corona na kuwa ugonjwa huo bado upo lakini hauwezi kukimbiwa ni  lazima tujifunze kuishi nao.
” Tunamshukuru sana Rais, Mhe.John Pombe Magufuli kwa kufanya maamuzi ya  kufungua anga ambapo tunaamini biashara ya Utalii na biashara ya anga zinategemeana kwa kiasi kikubwa.
Amesema uamuzi huo umeifanya biashara ya utalii kuweza kurejea kwa vile tayari mashirika ya ndege ya Ethiopia, Emirates, KLM na Quatar yameanza kuja nchini.
Naye, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto,  Dkt. Goldwin Mollel amewataka Wadau wa Sekta ya Utalii ikiwemo Wamiliki wa Hoteli kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na Wizara yake ili kuhakikisha usalama wa Wageni na wenyeji wanaowahudumia Watalii
Akizungumzia uamuzi huo wa kuifungua hoteli hiyo amesema  inatuma ujumbe kwa Wawekezaji wengine kuwa Tanzania ipo salama kwa i na Watanzani wapo tayari kwenda nchi za nje kwa ajili ya kutafuta shughuli za kibiashra.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo amesema tangu anga lilipofunguliwa kumeonesha dalili njema ya ujio wa idadi kubwa  ya watalii
” Kuna matumaini makubwa ya kupata watalii  wengi zaidi kwa mfano siku ya jana ndege ya Shirika la  KLM ilitua Uwanjaa  wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ( KIA) ikiwa na kabiria 200 kati ya hao 45 ni watalii waliokuja nchini kwa ajili ya kutalii” alisema Jaji Mstaafu Mihayo.
Amesema hiyo ni dalili njema  katika sekta ya Utalii nchini, ” Miezi mitatu iliyopita tulikuwa hatupokei watalii kabisa kwa hofu ya janga la Corona.

No comments :

Post a Comment