Kampeni ya usafi wa mazingira (National Sanitation Campaign) katika
halmashauri ya wilaya ya Handeni ambayo ilishindanisha shule za Msingi
na Sekondari imefikia kilele.
Mgeni
rasmi Bw. Francis Mashallo akitoa zawadi kwa washindi na kulia kwake ni
Afisa Elimu Sayansikimu ambaye ndiye alikuwa mratibu wa kampeni hiyo
Bi.
Grace Mbanga.
Kampeni ya usafi wa mazingira (National Sanitation Campaign) katika
halmashauri ya wilaya ya Handeni ambayo ilishindanisha shule za Msingi
na Sekondari imefikia kilelejumla walipewa vyeti.
Akizungumza katika kilele hicho mgeni rasmi Bw. Francis Mashalo alisema kuwa suala la usafi ni suala la kitaifa na lilianza tangu mwaka 1973 kwenye Azimio la Arusha. Halmashauri ya wilaya ya Handeni ilianza kampeni hiyo tangu mwaka 2012 na matokeo chanya yalionekana.
Pia aliwataka wananchi wadumishe usafi katika maeneo yao ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko na alisisitiza wananchi kujenga vyoo bora vinavyotumika na kuzingatia usafi wa vyoo hivyo bila kusahau kunawa mikono baada ya kutoka chooni pamoja na kuchemsha maji ya kunywa.
Naye Afisa Elimu Sayansikimu ambaye ndiye mratibu wa kampeni hiyo Bi. Grace Mbanga alitaja maeneo muhimu yaliyozingatiwa ili kupata washindi ambayo ni uwepo wa vyanzo vya maji safi na salama, usafi wa mazingira ya shule, utupaji salama wa taka, uelewa wa watu juu ya magonjwa ya mlipuko na dengu, uelewa wa suala la hedhi salama, ubunifu, kutambua njia na mbinu za kujikinga na magonjwa.
Aliongeza kuwa katika kampeni ya usafi wa mazingira kitaifa ya mwaka 2012 wizara nne zilishiriki katika kampeni hiyo ambazo ni wizara ya afya kama mdau wa afya ya jamii, wizara ya maji kama mdau wa miundombinu bora ya maji safi na salama, wizara ya elimu kama jamii lengwa na wizara ya TAMISEMI kama mtunga sera.
Naye mwalimu wa baiolojia wa shule ya sekondari Kwalugulu madam Winifrida Akhoguti alisema wamefurahia mafundisho yaliyotolewa na wataalamu pamoja na zawadi zilizotolewa ambapo italeta chachu na ari ya usafi wa mazingira pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuhusu suala la usafi wa mazingira.
Kwa upande wa mwanafunzi Said Mussa Msingwa aliahidi kutoa elimu hiyo ya usafi wa mazingira katika maeneo yao wanayoishi kwa wale ambao hawajapata elimu hiyo kwa kuwa uchafu wa mazingira unasababisha magonjwa ya mlipuko ambayo yanawaathiri watanzania wengi.
Washindi wa jumla ni pamoja na shule ya sekondari Kwankonje ambayo imeshika nafasi ya kwanza, shule ya msingi Nyasa ambayo imeshika nafasi ya pili na shule ya sekondari Kwalugulu ambayo imeshika nafasi ya tatu.
Mgeni rasmi Bw. Francis Mashallo akizungumza
Mratibu wa kampeni ya usafi wa mazingira Bi.Grace Mbanga akizungumza
Afisa Maendeleo ya jamii Bi.Thea Mauki akitoa elimu
Kitalu cha miti ambayo ni sehemu ya utunzaji wa mazingira shule ya Sekondari Kwalugulu
Mgeni rasmi Bw. Francis Mashallo akitoa zawadi kwa washindi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kwaluguru wakisikiliza mafunzo
No comments :
Post a Comment