……………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu,HESLB,
DAR ES SALAAM
KATIKA
kuhakikisha taifa letu linajenga uchumi ulio imara na jamii inayoheshimu
na kufuata
misingi ya uwajibikaji na ubunifu, Serikali pamoja na mambo
mengine imeendelea kuwekeza katika elimu ya juu.
Serikali
imeendelea kuhakikisha Watanzania wote wenye sifa wanapata elimu ya juu
kwa kupewa mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, iliyoanzishwa
chini ya kifungu cha Sheria Na. 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi
Julai, 2005.
Bodi ya Mikopo
pamoja na majukumu mengine, ina jukumu la kutoa mikopo au ruzuku kwa
wanafunzi wenye sifa na wahitaji wa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
na mwombaji stahiki na mhitaji anaweza kuomba mkopo /ruzuku ili
kugharamia sehemu ya gharama au gharama zote za masomo ya elimu ya juu.
Tangu kuingia
madarakani kwa Rais Dkt. John Magufuli, Serikali ya Awamu ya Tano
imeweza kuongeza bajeti ya maendeleo kutoka wastani wa asilimia 26 hadi
asilimia 40 na hivyo kuweza kupanua wigo na kuboresha upatikanaji wa
huduma za mbalimbali za jamii ikiwemo elimu ya Juu.
Katika kipindi
cha miaka mitano cha Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli Serikali
imeongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu kutoka Tsh. bilioni 348.7
mwaka 2014/2015 hadi Tsh. bilioni 450 mwaka huu wa Fedha 2019/2020.
Kutokana na
msukumo na juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali katika kuboresha elimu
ya juu nchini, Serikali imeiwezesha na kuijengea uwezo Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutekeleza vyema majukumu yake ya kisheria na
kuongeza uwazi na ufanisi katika upangaji, utoaji na ukusanyaji wa
mikopo.
Akiwasilisha
Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya mwaka 2020/2021,
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako anasema
katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20, Serikali kupitia Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu hadi kufikia machi 2020 imetoa
mikopo yenye thamani ya Tsh. Bilioni 449.99 kwa wanafunzi 132,119 sawa
na asilimia 99 ya fedha iliyoidhinishwa.
Prof. Ndalichako
anasema katika ya hao, wanafunzi 49,799 ni wa mwaka wa kwanza na 82,320
wanaoendelea na masomo hatua inayolenga kutoa fursa na kupanua wigo kwa
wanafunzi wenye sifa za uhitaji kujiunga na masomo katika vyuo na
taasisi za elimu ya juu nchini.
Kwa mujibu wa
Prof. Ndalichako anasema HESLB katika mwaka 2019/2020 pia imefanya
ukaguzi kwa waajiri 2,406 nchi nzima na kutambua wanufaika wapya 14,731
wenye mikopo iliyoiva yenye thamani ya Shilingi Bilioni 100.7 ambapo
kati yao wanufaika 13,969 (94%) wameanza kulipa.
‘Aidha, hadi
kufikia Disemba, 2019 idadi ya wanufaika wanaorejesha mikopo ilikuwa
imefikia 176,952 kati ya 184,166 waliotarajiwa sawa na asilimia 96 ya
lengo’’ anasema Prof. Ndalichako.
Kwa mujibu wa
Waziri Ndalichako anasema Bodi ya Mikopo imeendelea na ukusanyaji wa
mikopo iliyoiva ambapo kiasi cha Tsh. Bilioni 144.3 kati ya Tsh. Bilioni
166.1 zilizolengwa katika kipindi cha mwezi Juni 2019 hadi Machi 2020
sawa na asilimia 86.9 zimekusanywa, ambapo lengo la makusanyo kwa mwaka
lilikuwa ni kiasi cha Tsh. Bilioni 221.5.
Prof. Ndalichako
anasema katika kusogeza huduma ya mikopo ya elimu ya juu karibu na
wananchi pamoja na pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mikopo
iliyoiva, HESLB imefungua ofisi ya Kanda katika Mkoa wa Mtwara na
kufikisha jumla ya ofisi sita zilizopo katika Mikoa ya Dodoma, Mwanza,
Arusha, Mtwara, Mbeya na Zanzibar.
Akifafanua Zaidi
Prof. Ndalichako alisema Bodi ya Mikopo imeendelea kuboresha mifumo ya
uendeshaji ili kuongeza uwazi na ufanisi wa utoaji huduma katika
upangaji, utoaji na ukusanyaji wa mikopo iliyoiva, ambapo kwa sasa
mifumo hiyo inamuwezesha mwanafunzi kupata taarifa za mkopo wake kupitia
simu ya mkononi au mtandaoni na kuondoa usumbufu wa wanafunzi
kufuatilia taarifa hizo kwenye ofisi za Bodi.
‘Bodi imebuni
mfumo unaoviwezesha vyuo kuambatisha nyaraka muhimu kama vile matokeo ya
mitihani kupitia mtandao badala ya kutuma nakala ngumu, vilevile
uboreshaji wa mifumo umehusisha uunganishaji wa mifumo ya TEHAMA ya Bodi
ya Mikopo na ya Tume ya Vyuo Vikuu ambapo taarifa za udahili za
waombaji wa mikopo zinapatikana kwa urahisi na kwa wakati’’ alisema
Prof. Ndalichako.
Ni dhahiri kuwa
wigo wa utoaji elimu nchini unapanuka, hivyo ili kulinda ubora wa elimu
ni wajibu wa mamlaka zote zinazohusika na usimamizi na udhibiti wa ubora
wa elimu zitekeleze majukumu yao ipasavyo kwa kutoa miongozo na kufanya
kaguzi za mara kwa mara.
(Mwandishi ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi HESLB, anapatikana kwa ingayonga@heslb.go.tz)
No comments :
Post a Comment