………………………………………………………
Shirika lisilo la kiserikali la
Haki Madini limewajengea uwezo wachekechaji 60 wa madini ya Tanzanite wa
Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara juu ya elimu ya
afya na
usalama.
Afisa miradi wa shirika la Haki
Madini, Emmanuel Mbise akizungumza kwenye kijiji cha Naisinyai amesema
wachekechaji hao watapatiwa mafunzo hayo kwa muda wa siku mbili.
Mbise amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wanachangia kupunguza athari za afya kwenye shughuli za uchekechaji.
Amesema pamoja na kutoa mafunzo
hayo pia waliwapatia barakoa 400 kwa ajili ya kujikinga na vumbi wakati
wakifanya shughuli zao za uchenjuaji mchanga wa madini ya Tanzanite.
“Pamoja na washiriki hao 60 pia
kuna viongozi watano wakiwemo wa serikali hivyo kuwa na washiriki 65
ambao kwa namna moja au nyingine watakuwa mabalozi wazuri kwa wengine,”
amesema Mbise.
Mwenyekiti wa wachekechaji
wanawake wa Naisinyai, Nairukoki Leiyan amesema mashirika mengine yaige
mfano wa Haki Madini katika kuwajali wadau wa madini ya Tanzanite.
Leiyan amesema mafunzo hayo yatawasaidia kufanya shughuli zao ipasavyo na pia barakoa walizopatiwa zitawakinga na vumbi.
Mmoja kati ya wachekechaji hao
Isaya Maliaki amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo zaidi wa kufanya
kazi zao kwa usalama zaidi tofauti na awali.
Maliaki amesema pamoja na mafunzo
hayo pia barakoa waliopatiwa zitawakinga na vumbi wakati wakifanya
shughuli zao za uchenjuaji mchanga wa madini ya Tanzanite.
Amesema wachekechaji hao
wakitekeleza namna walivyofundishwa watakuwa salama kwani watakuwa
wanashika michanga kwa kutumia vikinga mikono wakati wakifanya kazi zao.
Afisa afya wa halmashauri ya
wilaya ya Simanjiro Boniface Jacob amewapongeza Haki Madini kwa
kuwajengea uwezo wachekechaji hao wa madini ya Tanzanite.
Jacob amesema zaidi ya kuwapa
mafunzo ya kuwezeshwa kujikinga na vumbi pia barakoa waliopatiwa
zitawakinga na vumbi na maambukizi ya virusi vya corona kwani wanapaswa
kuendelea kujikinga.
MWISHO.
Ofisa miradi wa shirika lisilo la
kiserikali la Haki Madini, Emmanuel Mbise akizungumza na wachekechaji wa
madini ya Tanzanite wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara, kwenye mafunzo ya siku mbili ya elimu ya afya na usalama kwa
wachekechaji.
No comments :
Post a Comment