Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Zainabu Chaula (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Bw. Shomari Omar (hayupo pichani) kabla ya
kuanza ziara ya kukagua vituo vya TEHAMA visiwani Zanzibar. Kulia kwake
ni Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Mawasiliano Dk. Jim Yonazi.
Kituo cha TEHAMA cha Mkokotoni
kilichopo Unguja, moja ya vituo sita vya TEHAMA vilivyokaguliwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano), Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Zainabu Chaula
kisiwani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jim Yonazi (wa kwanza kushoto) akiwa
na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Usafirishaji-SSerikali ya mapinduzi Zanzibar SMZ Bw. Shomari Omar kwa
pamoja wakifanya miamala ya T-Pesa kwenda kwa Msimamizi wa Kituo cha
TEHAMA Michweweni kuona utendajimkazi wa kituo hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano) Dk. Zainabu Chaula (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Naibu
Katibu Mkuu Sekta ya Mawasiliano Dk. Jim Yonazi (wa kwanza kushoto)
Mkurugenzi wa Utawala Kitolina Kippa (wa tatu kushoto) naMkurugenzi wa
Mawasiliano Mhandisi Clarence Ichwekeleza wakiwa wamewasili kisiwani
Pemba wakiwa tayari kukagua vituo vya TEHAMA vilivyojengwa na Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano) Dk. Zainabu Chaula (wa nne kushoto) akiwa pamoja na Naibu
Katibu Mkuu Sekta ya Mawasiliano Dk. Jim Yonazi (wa kwanza kulia) pamoja
na Mtendaji Mkuu UCSAF (wa pili kulia) watumishi wengine wa Sekta ya
Mawasiliano wakiwa Kiwanja cha ndege cha Abeid Amaan Karume wakiwa
tayari kuelekea Pemba kukagua vituo vya TEHAMA vilivyojengwa na Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano) Dk. Zainabu Chaula (wa nne kulia mstari wa mbele) akiwa
pamoja na Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Mawasiliano Dk. Jim Yonazi (kushoto
kwake) na kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Mawasiliano na Usafirishaji-Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, (SMZ) Bwana
Shomari Omar wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Kituo cha TEHAMA
Micheweni.
***********************************
Na Faraja Mpina – Zanzibar
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Jamhuri nya Muungano
ya Tanzania, Dkt. Zainabu Chaula ameelekeza kuwa vituo vya TEHAMA
vilivyojengwa Zanzibar na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF)
kujiendesha
kibiashara badala ya kutoa huduma bure kwa wananchi, ili
kuweza kumudu gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kuleta faida kwa
Serikali.
Dkt. Chaula aliyasema hayo
mwanzoni mwa wiki hii alipokuwa katika ziara yake ya kwanza ya kikazi
visiwani Zanzibar kukagua vituo 10 vya TEHAMA vilivyojengwa na Mfuko
wa Mawasiliano kwa wote nchini UCSAF. Vituo hivyo viko 10 Unguja vituo 4
viko Pemba.
“Tusiwe waumini wa vitu vya
bure, dhumuni la Serikali kufanya uwekezaji huu sio kupata hasara ila ni
kusogeza huduma kwa wananchi kwa matarajio ya uwekezaji huo utaweza pia
kujiendesha, kufanya maboresho na kuleta faida kwa Serikali”, alisema
Dkt. Chaula kwa msisitizo.
Aidha Dk.t Chaula amewataka
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) pamoja na Shirika la Posta (TPC)
kuwa wabunifu kwa kuweka huduma zao katika vituo hivyo vya TEHAMA kama
vile miamala ya T-Pesa, kuuza vocha na laini za simu pamoja na huduma za
Posta mtandao huku akiwaasa wataalamu kutumia taaluma zao kuwashauri
vizuri viongozi katika maeneo yao ya kazi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi, na Usafirishaji-Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bwana Shomari
Omar, amekiri kuwa Dkt Chaula amewafumbua macho kwasababu hapo awali
hawakuwa na mtazamo wa kibiashara katika matumizi ya vituo hivyo vya
TEHAMA ambavyo vimejengwa kwa gharama kubwa na Serikali.
“Iwapo vituo hivi vitatoa huduma
bora za mawasiliano na intaneti yenye kasi kubwa, wananchi watakuwa
tayari kutumia na kulipia gharama za huduma hiyo, hii itasaidia kupoteza
kabisa dhana ya kuviendesha vituo hivi kwa hasara”, alisema Bwana Omar.
Nae Meneja wa TCRA Ofisi ya
Zanzibar, Esuvatie Massinga amesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) ndio msimamizi na mdhibiti wa Mawasiliano na wanajipanga
kuhakikisha wanaweka programu maalum zitakazozuia wanafunzi na wateja
kuangalia picha za ngono ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa vituo hivyo
havitatumiwa kuvunja sheria za matumizi salama ya mtandao.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF) Bi. Justina Mashiba ametoa taarifa
mbele ya ujumbe wa Katibu Mkuu kuwa gharama za ujenzi wa kituo kimoja
cha TEHAMA umegharimu kiasi cha shilingi milioni 113 na makadirio ni
kituo kimoja kuingiza faida ya zaidi ya shilingi milioni sita kwa mwaka
iwapo vitasimamiwa vizuri na waendeshaji wa vituo vivyo vya kisasa vya
mawasiliano.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Mawasiliano wa Serikali ya
Muungano ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano Dkt.
Jim Yonazi, Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano injinia Clarence
Ichekweleza na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Bibi Kitolina Kippa.
Wengine katika msafara wa Katibu Mkuu wa kukagua vituo hivyo vya TEHAMA
Zanzibar ni pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
nchini Bi. Justina Mashiba, Kaimu Mkuu wa Manunuzi bibi Lightness
Makundi, Mwanasheria Eunice Masigati wa Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) pamoja na watumishi wengine wa Wizara
na Mfuko wa mawasiliano kwa Wote.
No comments :
Post a Comment