Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisisitiza jambo wakati wa mazunguzo na daadhi Wananchi waliojitokeza wakati wa ziara
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt.
Damas Ndumbaro amefanya ziara katika eneo la mpaka wa Mkenda uliopo
Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma unaoinguanisha Tanzania na nchi
Jirani ya Msumbiji.
Ziara hii inalenga kibaini na kutatua changamoto
mbalimbali ili kukuza biashara na uhusiano wa kidiplomasia baina ya
Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji. Katika ziara hiyo Dkt. Ndumbaro
aliambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ikiongozwa na Mkuu
wa Wilaya ya Songea Mjini Mhe. Pololet Mgema.
Akiwa mpakani
hapo Dkt. Ndumbaro amefanya mazungumzo na watumishi wa Idara mbalimbali
za Serikali walipo katika ofisi za mpaka huo kwa lengo la
kusikiliza changamoto na mapendekezo yanayolenga kuboresha namna ya
utoaji huduma kwa wakazi wa eneo la mpaka na watumiaji wa mpaka huo.
Aidha, Dkt. Ndumbaro pamoja na kutoa ufumbuzi wa baadhi ya changamoto,
na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizosalia amewataka watumishi
kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu, jitihada na uaminifu.
Dkt.
Ndumbaro pia ametembelea Ofisi za mpakani kwa upande wa Nchi jirani ya
Msumbiji na kufanya mazungumzo na Watumishi walipo katika Ofisi hizo.
Mheshimiwa
Ndumbaro, amewaleza wakazi na watumishi walipo mpakani humo kuwa
Serikali inanendelea na hatua za kuzitatua changamoto kubwa zinazo
changia ugumu wa utekelezaji wa majukumu ya kilasiku na kuadhiri
mwenendo wa biashara mpakani hapo, ikiwemo ukosefu wa umeme, huduma ya
mawasiliano na barabara ya kiwango cha lami.
Dkt.
Ndumbaro amewapongeza Watumishi walipo mpakani kwa kazi nzuri
wanayoifanya na amewahimiza Watumishi hao kuendelea kutekeleza Dilomasia
ya Uchumi, kuendeleza uhusiano mwema na kushughulikia suala la Diaspora
|
No comments :
Post a Comment