Mkuu wa Idara ya Huduma za Kifedha
kwa Biashara za Kimataifa wa Benki ya NMB – Linda Teggisa, akizungumza
wakati mabalozi wa nchi nane (Misri, Pakistani, Uturuki Kenya, Uganda,
Falme za Nchi za Kiarabu na Sweden) wanaoziwakilisha nchi zao hapa
nchini walipotembelea Banda la Benki ya NMB kwenye maonyesho ya Saba
saba.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni
cha Urusi- Rifat Pateev akizungumza na Ofisa wa Benki ya NMB – BatuIi
Sunna wakati mabalozi wa nchi kumi wanaoziwakilisha nchi zao hapa
nchini walipotembelea Banda la Benki ya NMB kwenye maonyesho ya Saba
saba.
………………………………………………………………………….
Benki ya NMB inaupa uwezeshaji na
ushirikishaji wazawa kipaumbele katika kuchangia kwake utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo humu nchini, hasa ile endelevu ya
kimkakati iliyoanzishwa na Serikali.
Sera hii ya benki hiyo ambayo
pia inatumika kwenye kufadhili uwekezaji, ni mpango wake wa makusudi
kusaidia uendelezaji na ushiriki wa Watanzania na biashara zao katika
ujenzi wa taifa na maendeleo yake kwa ujumla.
Hiyo ni kwa mujibu wa Mkuu wa
Idara ya Huduma za Kifedha kwa Biashara za Kimataifa wa Benki hiyo – Bi.
Linda Teggisa, aliyetoa ufafanuzi huo baada ya kuupokea ujumbe wa
Mabalozi nane walioambatana na uongozi wa Chemba ya Wafanyabiashara,
wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) walipotembelea banda la Benki
ya NMB kwenye Maonyesho ya Saba Saba ambayo yanafungwa rasmi leo.
Bi. Linda aliufahamisha ugeni
huo kwamba, pamoja na kuwahudumia wageni wanapokuja Tanzania kuwekeza na
kushiriki katika miradi mbalimbali, maendeleo ya wazawa yanapewa
kipaumbele kikubwa na benki yao. Alisema swala la kuwawezesha Watanzania
ili washiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na
mikubwa ni la msingi sana kwa Benki ya hoyo inayojivunia kuwa na
rasilimali zenye thamani ya takribani shilingi trioni 6.5 pamoja na
amana zipatazo shilingi trioni 4.7.
“Kwa ufupi sisi kama Benki
kubwa nchini tunatoa huduma za kifedha ambazo zinahusisha sekta
mbalimbali na miradi nyeti kama sekta ya kilimo, uchukuzi, nishati,
maendeleo ya miundombinu pamoja na zile za afya na elimu. Lakini pia
mfano mzuri wa uwezeshaji wa wazawa ni ule wa wakandarasi wa humu
nchini.” Alisema Linda.
Mtaalamu huyo wa NMB aliwaambia
mabalozi hao kutoka Misri, Pakistani, Kenya, Uganda, Falme za Nchi za
Kiarabu na Sweden ambazo ni moingoni mwa nchi ambazo kampuni zao
zinashiriki katika kutekeleza miradi ya kimkakati kuwa, Benki yao ina
jukumu la kuwahudumia wenyeji lakini pia kuhakikisha kuwa
wafanyabiashara na wawekezaji wa nje nao wananufaika na huduma zao bora
za rejareja na zile za wateja wakubwa.
Bi. Teggisa alilifafanua hilo kwa
kueleza jinsi Benki ya NMB inavyoshiriki katika utekelezaji wa miradi
mikubwa ya kimkakati kwa kumsaidia mkandarasi mkuu wa mradi wa Ujenzi wa
Reli ya Kisasa (SGR), kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki ambayo balozi
wake hapa nchini alikuwa kwenye msafara wa TCCIA uliotembelea banda la
benki hiyo.
Uwekezaji huu mkubwa wa kipekee
kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania na uwezeshaji wa kuigwa, ndiyo
uliyoifanya TCCIA na ujumbe wake wa mabalozi nane kati ya kumi iliyokuwa
imewaalika kutembelea Saba Saba ya mwaka huu kufika katika banda la
Benki ya NMB.
Rais wa chemba ya TCCIA, Bw. Paul
Koyi, aliishukuru Benki ya NMB kwa kuyapa kipaumbele maslahi ya
Watanzania na kuongoza kuchangia maendeleo ya nchi.
No comments :
Post a Comment