Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa
BancABC, Barton Mwasamengo akiwasikiliza maafisa wa benki hiyo Advera
Ruhiye (Kushoto) na Mariam Haji kuona namna wanavyowahudumia wateja
wakati wa maonyesho ya 44 ya biashara ‘Saba Saba’ yanayoendelea jijini
Dar es Salaam.Benki hiyo inatoa huduma mbalimbali za kibenki ikiwamo
mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs).
Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa
BancABC, Barton Mwasamengo akizungumza na mmoja wa wateja waliotembelea
banda la benki hiyo katika maonesho ya biashara ya Saba Saba
yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Benki hiyo imejidhatiti katika
kuendeleza biashara ndogo ndogo na za kati kwa kutoa mikopo yenye riba
nafuu.Kushoto kwake ni Meneja Mahusiano wa benki hiyo Charles Silayo.
Maafisa wa BancABC,Hope Madiavalle
(Kushoto) na Shazman Karim wakitoa maelekezo kwa wateja waliofika
kwenye banda la benki hiyo katika Maonesho ya 44 ya biashara maarufu
kama SabaSaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.Benki hiyo imejidhatiti
katika kuhakikisha inatoa huduma zenye ubora ikiwamo kutoa mikopo yenye
riba nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.
…………………………………………………………………
Dar es Salaam.
Benki ya ABC (BancABC) imeshiriki
maonesho ya 44 ya biashara maarufu kama
Sabasaba ambapo benki hiyo
imeeleza namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za kibenki hasa
utoaji wa mikopo nafuu kwa wateja wake.
Maadhimisho hayo yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa.
Akizungumza kwenye maonyesho
hayo, Mkuu wa Kitengo cha hazina wa benki hiyo, Barton Mwasamengo
alisema benki imejidhatiti katika kuhakikisha inaboresha maisha ya
watanzania wengi kwa kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.
“Tunatoa mikopo kwa
wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na mikopo binafsi kwaajili ya
kuendeleza shughuli ndogondogo kama mamalishe, boda boda na wengine
wengi, BancAbc ipo kwaajili ya watanzania wote,” alisema Mwasamengo.
Mwasamengo alisema katika
kuboresha huduma imefanikiwa kutoa huduma za kibenki za kidigitali
ambapo wateja wanaweza kufanya malipo mtandaoni kwa urahisi zaidi.
Mwasamengo alisema benki hiyo
imechukua hatua mbalimbali ili kutoa unafuu kwa wateja wake kutokana na
athari za mlipuko wa ugonjwa wa Corona ikiwamo kutoa unafuu wa riba kwa
wateja waliokopa.
“Sisi kama benki tumefungua
milango kwa wateja wetu wote waliokopa na ambao hawajakopa, tunataka
kuwaendeleza wateja hasa kwa kusikiliza changamoto zao na tumeendelea
kuchukua hatua mbalimbali ikiwamo kutoa unafuu wa riba,” alisema.
Vilevile, benki hiyo imeahidi
kushirikiana na Serikali katika kuendeleza agenda ya ujumuishwaji wa
watu kiuchumi yaani ‘Financial Inclusion’ kwa kuwasaidia wajasiriamali
wadogo na wa kati kupitia mikopo yenye riba nafuu.
Pamoja na huduma nyingine,
benki hiyo ina akaunti ambayo inampa mteja uhuru wa kupokea riba kuanzia
riba ndogo kabisa ya Sh10,000 pasipokuwapo na makato ya kila mwezi.Hii
imewezekana kupitia mtandao wetu wa kibenki unaowahudumia watanzania
nchi nzima.
Aliwahimiza watu kutembelea katika banda la BancABC ili kujionea huduma mbalimbali.
No comments :
Post a Comment